Hivi ndivyo Polisi walivyomkamata aliyeweka video ya Mwarabu anayempiga Mhindi

 
Mtu mmoja amekamatwa Dubai kwa kuweka video (imepachikwa hapo chini) kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo inamwonesha Mwarabu mmoja aliyeonekana kukasirika akirusha maneno huku akimkung'uta kwa kutumia "igal" Mhindi mmoja barabarani. Kama vile hiyo haitoshi, pia alikuwa akimsunda makonde kifuani/tumboni. Baadaye anamlazimisha Mhindi kwenda kwenye gari lake kabla ya kumrudisha tena ambapo mtu mwingine kutoka kwenye gari jingine anaonekana kuingilia kati, kitendo kinachosababisha Mwarabu aamue kuiweka igal yake na kuivaa kichwani.
Polisi walipata taarifa kutoka kwa mtoto wa Mwarabu akilamika kuwa video hiyo inamdhalilisha baba yake.

Baada ya vyombo vya habari kuchapisha taarifa hiyo na watu kuhoji sababu ya mtuhumiwa aliyekuwa mpita njia tu aliyeona tukio hilo na kuamua kurekodi, kutiwa mbaroni, Polisi wa Dubai katika ukurasa wao wa kijamii wa Twitter wameandika na kutetea uamuzi wao kuwa sababu ya kumkamata mtuhumiwa si kwa kurekodi video, bali kwa kuiweka kwenye mtandao wa kijamii na kuwashirikisha wengine. 

Wamesema mtuhumiwa alipaswa kuipeleka video hiyo polisi. Soma maelezo hayo kwenye "screen-shot" iliyobandikwa hapo chini baada ya video ya tukio hilo.
Picture 

Post a Comment

Previous Post Next Post