Israel na Palestina kuendelea na mazungumzo ya amani baada ya miezi miwili

John Kerry delivers remarks on the Middle East Peace Process Talks, with Israeli Justice Minister Tzipi Livni and Palestinian chief negotiator Saeb Erekat.


Na Flora Martin Mwano

Israel na Palestina watakutana tena katika kipindi cha miezi miwili ijayo kuendeleza jitihada za kusaka suluhu ya mzozo wao uliodumu kwa muda mrefu.

Mpatanishi wa mgogoro wa Israel na Pelestina, John Kerry (katikati) akiwa na wawakilishi wa pande zote jijini Washington. REUTERS/Jonathan Ernst

Mpatanishi wa mzozo huo Waziri Mkuu wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema mkutano ujao wa wawakilishi wa pande hizo utafanyika nchini Israel au Palestina kutokana na watakavyokubaliana.

Akiongea baada ya kumalizika kwa siku mbili za mazungumzo jijini Washington, Kerry ameeleza kuwa pande zote zimejidhatiti katika kujadili maswala muhimu ili kupata suluhu inayokusudiwa.

Kerry amesema ingawa changamoto ni kubwa lakini huu ni wakati muafaka kwa majirani hao kupatana baada ya kuzozana kwa kipindi kirefu.

Awali Rais wa Marekani, Barack Obama alikutana na wajumbe wa Israel na Palestina wanaoshiriki mazungumzi hayo, Isarel inawakilishwa na Waziri wake wa Sheria Tzipi Livni na Palestina inawakilishwa na Saeb Erekat.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza, Mjumbe wa Israel Livni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya mchakato huo.

Katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, Kerry amefanya ziara sita tofauti katika eneo la Mashariki ya Kati akihimiza pande zote kukubali kurejea katika mazungumzo hayo ambayo yaliyovunjika mwezi Septemba mwaka 2010.

Post a Comment

Previous Post Next Post