STAA wa
filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la
presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani
linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.
Akizungumza hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa
muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini
likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.
“Kwa
kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa
duniani, unajua wakati mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu
nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!” alisema Wolper
Post a Comment