
Gazeti la Sunday Mirror limebainisha kuwa Drogba alizuru Cobham Jumatatu iliyopita na akazungumza na Mourinho, ingawa kiini cha mazungumzo yao kimebaki kuwa siri.
Inaelezwa kuwa Mourinho ana nia ya kumsainisha nyota huyo wa miaka 35 kwa ajili ya msimu huu, lakini Chelsea italazimika kwanza kuishawishi klabu yake ya Galatasaray.
Kama miamba hiyo ya Uturuki haitamruhusu kuondoka au Drogba anataka kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki, basi Mourinho atampa ofa ya kukipiga tena Chelsea msimu ujao.
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich alijaribu kumsajili tena Drogba Januari mwaka huu na atakuwa tayari kumkaribisha tena mshambuliaji huyo wa zamani wa Marseille akiwa kwenye uwezo wowote ule.
Wiki iliyopita, Mourinho akizungumza kuhusu ushawishi wa Drogba unavyoweza kukisaidia kikosi chake alisema: “Naweza kumtumia Didier kama mfano kuweza kuwashawishi nyota vijana kunisikiliza kwa sababu alinisikiliza mimi kutoka siku ya kwanza.”
Mourinho alimsajili Drogba kuichezea Chelsea na raia huyo wa Ivory Coast alipiga mabao 157 kwa zaidi ya miaka nane aliyokuwapo Stamford Bridge.
Baada ya kutembelea Cobham, Drogba aliungana na wachezaji wake wa Galatasaray katika kambi yao ya maandalizi ya msimu huko St George’s Park
Post a Comment