Mahakama
ya Vietnam imewahukumu watu watano adhabu ya kifo baada ya kukutwa na
hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya
heroin nchini humo.
Shirika la habari la nchi hiyo limesema wanaume watatu na wanawake
wawili wamehukumiwa adhabu ya kifo huko Bac Giang, Vietnam kwa kukutwa
na kilo 78 za dawa za kulevya aina ya Heroin, na watu wengine wanne wiki
iliyopita walikutwa na hatia kwa kosa kama hilo. Mpaka sasa idadi ya
watu 500 waliokutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya ‘unga’ wako
katika foleni ya adhabu ya kifo kwa makosa ya kujihusisha na dawa za
kulevya nchini humo.
Biashara ya dawa da kulevya inaonekana kushamiri kwa kasi katika nchi
nyingi duniani ikiwemo Tanzania, ambayo siku chache zilizopita raia
wake wawili wasichana walikamatwa
nchini Afrika kusini na karibia kilo 150 za dawa za kulevya aina ya
Crystal methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya shilling billion 6.
SOURCE: SABC

Post a Comment