KOCHA WA TAIFA STARS AZUNGUMZIA MECHI YAO NA UGANDA


Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Tansoma kuelezea maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Afrika Kusini mwakani. 

Poulsen amesema kikosi kimejiandaa vizuri na kitautumia uzoefu kilioupata katika michezo ya kufuzu kwenda kombe la dunia kama motisha kitakapokabiliana na Uganda kesho. 

Poulsen amewasisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taigfa kuishangilia timu yao kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Ivory Coast.

Post a Comment

Previous Post Next Post