Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameelezea upinzani wake
mkubwa dhidi ya mapinduzi ya kijeshi nchini Misri yaliyomuondoa
aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Mursi, akiita hatua hiyo kuwa
'haramu.'
Akielezea matukio ya hivi karibuni nchini Misri jana
Alhamisi, Erdogan alisema kuwa Uturuki inayachukuliwa mapinduzi hayo
kuwa "haramu," shirika rasmi la habari la Anadolu liliripoti.
“Kila mapinduzi ya kijeshi, bila kujali malengo, nchi na sababu yake,
ni unyongaji wa demokrasia, watu na mustakbali wa nchi," Erdogan alisema
na kuongeza kuwa maandamano ya kuipinga serikali mjini Cairo
hayakuhalalisha mapinduzi hayo.
Misri ilitumbukia katika
machafuko na ghasia baada ya jeshi kumuondosha Mursi, kusitisha matumizi
ya katiba, na kulivunja bunge mnamo Julai 3. Jeshi lilichukua hatua
hiyo kufuatia siku kadhaa za maandamano ya kumpinga Mursi.
Tarehe 4 Julai jeshi lilimtangaza mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba, Adly Mansour, kuwa rais wa mpito.
Wziri Mkuu huyo wa Uturuki aliongeza kuwa, “iwapo viwanja ndio dalili,
vipi kuhusu uwanja wa Rab’a Al-Adawiya?” akimaanisha uwanja ulio jirani
na makao ya rais wa Misri, ambapo wafuasi wa Mursi walikuwa
amekusanyika.
Julai 5, Erdogan alilaani hatua ya kuondolewa
Mursi madarakani kwa jeshi kuingilia kati na kuzikosoa nchi za Magharibi
kuwa kushindwa kuiona hatua hiyo kuwa ni mapinduzi.
Tangu wiki
jana, Misri imekuwa ikishuhudia maandamano na makabiliano
yanayowahusisha wafuasi na wapinzani wa Mursi na vikosi vya usalama.
Watu wengi wameuawa kwa siku kadhaa zilizopita huku zaidi ya watu 80
wakiripotiwa kuuawa Julai 8 pekee.
Julai 10, serikali ya Misri
inayoungwa mkono na jeshi ilishadidisha mbinyo dhidi ya chama cha Muslim
Brotherhood, kwa kutoa amri ya kukamatwa kwa kiongozi wake wa kiroho,
Mohamed Badie na maafisi wengine waandamizi.
Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea wasiwasi wake kuhusu
kushikiliwa kwa wanaharakati wa kisiasa nchini Misri na kusema kuwa,
“kufanya ubaguzi kwa chama au jamii yoyote ni jambo lisilokubalika.
Post a Comment