
Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
William Burns amewasili mjini Cairo Misri tayari kwa mkutano na
viongozi wa serikali ya mpito wanaoungwa mkono na jeshi. Ni Ziara ya
kwanza kufanywa na afisaa mkuu wa Marekani tangu jeshi kumwondoa
mamlakani aliyekuwa rais Mohamed Morsi tarehe 4 Julai.Duru kutoka Ikulu
ya rais Marekani, zinasema kuwa Burns atashinikiza kumalizwa kwa ghasia
na vurugu na kuundwa kwa serikali ya pamoja ya viongozi wa kiraia
watakaochaguliwa kidemokrasia. Awali mwendesha mkuu wa mashtaka alipiga
tanji mali za viongozi 14 wa kiisilamu.
Kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood
Mohammed Badie na naibu wake Khairat al-Shater wanaripotiwa kuwa
miongoni mwa waliokamatwa. Hatua hiyo ni sehemu ya uchunguzi kuhusu
madai ya uchochezi, yaliosababisha ghasia za kisiasa nchini humo. Mamia
ya watu wamefariki wakati wa maandamano yaliyofanywa na mahasimu wa
kisiasa kati ya wale wanaomuunga mkono Morsi na wapinzani wake, katika
wiki mbili zilizopita. Wakati huohuo maafisa wanasema kuwa washukiwa wa
chama cha Brotherhood, wameshambulia basi lililokuwa linawabeba
wafnyakazi wa kiwandani Kaskazini mwa Sinai huku wakiwaua watu watatu
Post a Comment