Watoto
mapacha wa kiume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika
mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea.
Madaktari wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao
ambao wamezaliwa Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao
imetengana wakati uti wa mgongo umeungana na pia wanashare sehemu ya
ubavu.
Dr. S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni
nadra sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama
‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea
India.
Daktari huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye
‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea
kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa
kuokoa maisha ya mapacha hao.
Tatizo kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan
mwaka (2011) ambao waliozaliwa wakiwa wameungana vichwa. Watoto hao
Rital na Ritag Gaboura walifanikiwa kutenganishwa salama japo kwa tatizo
kama lao uwezekano wa kupona hua ni kwa mmoja kati ya million kumi.
Rital na Ritag Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa
Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa
Post a Comment