
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya
uhamiaji wakati alipowasili kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea
kuweka jiwe la msingi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20,
2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati
alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji Samaki cha Ruhila
kilichopo mjini Songea. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.

Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea
Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea
Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma. Wapili kulia ni mkewe, Mama
Tunu Pinda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama moja ya magari ya mafunzo yanayotumika
katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati
alipokizindua chuo hicho.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (wapili kuhoto) wakitazama vyakula na
vifaa mbalimbali vya jikoni katika maonyesho ya kozi zinazofndishwa na
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati
alipokizindua Julai 20, 2013.
anachuo
wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Tanzania (VETA) ambao majina
hakupatikana wakionyesho mavazi yanayoshonwa na wanachuo wa Chuo hicho
kabla ya mgeni rasmi Waziri Mkuu , Mizengo Pinda alipozindua Chuo chao
mjini Songea Julai 20, 2013. Mheshimiwa Pinda alikuwa katika ziara ya
mkoa wa Ruvuma.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakisalimiana na madiwani wa Manispaa
ya Songea wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa
hadhara mjini Songea akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto kwake) wakitazama ngoma ya
wanawake wa Songea kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafnzi wa Shule ya Sekondari ya
Songea Girls baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai
20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Baadhi
ya Waislamu wa Songea wakishiriki katika futari wakati Waziri Mkuu,
Mkuu Mizengo Pinda alipofuturisha kwenye Ikulu ndogo a ya Songea akiwa
katika ziara ya mkoa wa Ruvuma jana.
Baadhi
ya Waislam walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kwenye Ikulu ndogo ya Songea wakishiriki katika futari
hiyo.

Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wapili kulia) akizungumza na baadhi
ya wanawake walioshiriki katika futari ambayo Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda aliwaandalia baadhi ya Waislam wa Songea Julai 20, 2013. Alikuwa
katika ziara ya mkoa wa Ruvuma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu








Post a Comment