
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya
watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha
shimo.


Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu
ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Rukia Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi
akitolewa nje ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5
Jela
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni
Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni
kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Na Mbeya yetu
Post a Comment