MWENYEKITI WA CCM AJINYONGA MKOANI TABORA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Tabora mstaafu amefariki Dunia baada ya kujinyonga akiwa chumbani kwake Mjini Tabora.

Mwenyekiti huyo Jaffary Ally, aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa TANU Mkoani Tabora,amejiua akiwa nyumbani kwake katika eneo la Ipuli Manispaa ya Tabora. Sababu za kujiua bado hazijulikani.

Mzee Ally anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 80 na alikutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia waya wa simu.

Inaelezwa kuwa Mke wake ndie aliyekuwa wa kwanza kumkuta amejinyonga majira ya saa kumi jioni juzi na kutoa taarifa kwa majirani akipiga mayowe.

Kwa mujibu wa majirani wa mzee huyo,inaelezwa hakuwa nyumbani kwake bali kwa mmoja wa watoto wake baada ya
kupata ajali ya pikipi na kulazwa kwa wiki moja katika Hospitali ya Mkoa Tabora,kitete.

Marehemu alijinyonga siku moja tu baada ya kuwasili nyumbani kwake tukio ambalo limewashangaza wananchi kwani alikuwa bado ni kiongozi.
 
Marehemu hadi nafariki alikuwa ni Mwenyekiti wa wazee wa Kata ya Ipuli na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere yalipo makazi yake.

Marehemu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora,Moshi Omary Nkonkota,alisema marehemu aliwahi kushika wadhifa alionao miaka ya nyuma huku akiwa bado ni tegemeo kwa Chama cha Mapinduzi na kusikitishwa na lililotokea.

Polisi Mkoani Tabora limeeleza linachunguza kifo hicho ili kujua chanzo cha hatua iliyochukuliwa na marehemu.

Post a Comment

Previous Post Next Post