Mrembo
na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti
zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa
ameshangazwa mno na taarifa hizo.
Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi
yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”
Bongo5 imezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu
wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na
mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.
Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.
“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe
kuangalia chochote. Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya
nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya
kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani. Kiukweli sijapenda, yaani
bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo,
si suala zuri,” amesema Linah.
Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.
“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na
boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia
amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.Nashindwa
kuelewa, kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua
source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true,
lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho,
nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”
Msikilize zaidi Linah hapo chini.
Hata hivyo, tumempigia simu Kalapina kumuuliza habari hizo zimetoka
wapi na yeye kuendelea kusema kuwa habari hizo zimeenea maeneo mengi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu wanaendelea kudai ni habari za
kweli
Credit:- Bongo5

Post a Comment