Njiwa akiwa na ujumbe wa barua kama inavyo onekana
Njiwa akiwa amedhoofu kwa Baridi akiwa katika choo cha wanaume
Hii ni sehemu alipokutwa Njiwa huyo
Majengo nje ya Ofisi ya Afisa Mwajiri
Baadhi ya wafanyakazi wakielekea eneo la tukio
Afisa Mwajiri (Mwenye shati ya bluu) Na baadhi ya wafanyakazi wakishuhudia tukio
Mashuhuda wakitoka eneo la tukio
Barua iliyoletwa na Njiwa maeneo ya Ofisi ya Mwajiri upande wa mbele na nyuma
Jengo la Ofisi ya Afisa Mwajiri
Stesheni ya TAZARA kituo cha Mbeya
ANGALIZO: UNAPOTUMIA HABARI HIZI USIPOTOSHE UKWELI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0787-490 752 Au 0654-221465
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU
*******************************************************
WAFANYAKAZI
wa Mamlaka ya Reli, kati ya Tanzania na Zambia(TAZARA) jana walijikuta
katika wakati mgumu na baadhi yao kulazimika kuzikimbia ofisi zao, baada
ya ndege aina ya njiwa kukutuwa katika moja ya choo cha ofisi hiyo
akiwa amefungwa hirizi shingoni, huku akiwa na barua yenye ujumbe wa
onyo kali.
Tukio
hilo la aina yake, lilitokea mapema leo saa mbili asubuhi katika
ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Iyunga Mkoani hapa, hali ambayo
mbali na baadhi ya wafanyakazi wake kuzikimbia ofisi, ilisababisha
kuibuka kwa mjadala mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Mtandao
huu ulifanikiwa kushudia njiwa huyo mweusi akiwa nyuma ya choo cha
kiume katika eneo hilo la ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi
shingoni iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni
Nyekundu, Njano na Nyeupe.
Mbali
ya kuwa na hirizi hiyo, pia njiwa huyo alikuwa amebeba barua inayodaiwa
kuwa ni ya mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (jina limehifadhiwa kwa
sababu maalumu) ambaye anadaiwa hivi karibuni kufukuzwa kazi kwa makosa
ya ubadhirifu.
Barua
hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha
mbili za Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili
yalisomeka “ Naomba majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini”
ilisema sehemu ya ujumbe huo, huku ikiwa na orodha ya majina matatu ya
viongozi wa shirika hilo.
Mbali
na ujumbe huo ukiwa umeandikwa kwa maandishi ya mkono yaliyokolezwa kwa
wino mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na
maandishi yakiwa ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi
huyo.
Akizungumzia
tukio hilo, Mwajiri wa mamlaka hiyo kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha
kwa jina la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba
waliobaini ni wahudumu wa usafi.
Aliongeza
kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu na wafanyakazi wenzake
ambao walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika
huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho.
Alisema
baada ya kushuhudia hali hiyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi
kilichopo ndani ya shirika hilo, ambapo waliichukua barua hiyo na baadhi
ya wafanyakazi hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.
“Kwa
kweli hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa siwezizungumzia chochote kwa
kuwa hata mimi tukio hili limeniweka katika wakati mgumu na nimeshindwa
kuendelea na majukumu yangu ” alisema Mgweno.
Hata
hivyo kuliibuka malumbano makali kati ya wafanyakazi wa shirika hilo
walioshuhudia tukio hilo, ambapo baadhi yao wakidai kuwa tukio hilo ni
la kutengenezwa kwa lengo la kuchafuana.
“Hebu
angalia hiyo barua yenyewe mbona ni kivuli (Photocopy), kama ingekuwa
ni ya ….wanamtaja mfanyakazi aliyefukuzwa jina limehifadhiwa ingekuwa ni
nakala halisi….haiwezekani mambo haya ni kutaka kuchafuana tu” alisema
mmoja wa wafanyakazi hao.
Lakini baadhi yao wakiamini kweli kuwa barua hiyo ilitumwa ili itoe vitisho kwa viongozi wa shirika hilo.
Baadhi
ya askari polisi wa kituo cha Tazara walikiri kutokea kwa tukio hilo na
kwamba wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wake.
“Ndugu
zangu nyie mnajua taratibu za utoaji wa taarifa kwa jeshi hili, maana
wapo wahusika, lakini kwa kifupi sisi tulipokea taarifa na tunaendelea
kuzifanyia kazi” alisema mmoja wa askari hao.
Hata hivyo, hadi tunapoondoka eneo la tukio majira ya saa sita mchana Njiwa huyo alikuwa bado yupo eneo la tukio.
Chanzo: Mbeya yetu Blo

Post a Comment