
Ray mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI,
mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi
‘Ray the Greatest’ hivi karibuni aliangusha bonge la sherehe ya siku
yake ya kuzaliwa na kuwakaribishwa rafiki zake na wadau wa filamu katika
moja ya Hotel, siku hiyo pia aliweza kumkumbuka swahiba yake marehemu
Kanumba na kuhisi uenda angekuwepo siku hiyo.
.
.

Maswahiba wawili wakitoka safari marehemu Kanumba na Ray

Ray akiwa na mdau wa filamu Inno.
“Ni
siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa
karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana
katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku
kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya
Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe
kwa amani Amen,” alisema The Greatest.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao
ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana,
JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo
kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio
kama hayo.
.
.
![]() |
| Ray akiwa na marehemu katika filamu ya Oprah |
Pengine
sasa watu wanaona tasnia ya filamu kupwaya baada ya Ray kukosa mpinzani
wa kweli katika tasnia ya filamu, tofauti na alivyokuwepo marehemu
Kanumba ushindani wa mafanikio ulikuwa wazi kuanzia ubora wa kazi na
umiliki wa mali ikiwa sambamba na magari mazuri, vifaa vya Production
jambo ambalo kwa sasa analifanya Ray pekee hana mpinzani

Post a Comment