ROHO MKONONI 17

Photo: ROHO MKONONI
MTUNZI: George Iron

SEHEMU YA KUMI NA SABA

 Na kwa nini alimtuma Fonga kumfuatilia siku ile ili asifanye mapenzi na Isaya?
Swali hili lilimshtua sana Fonga. Siku yeye alipoagizwa kumfuatilia Betty nd’o siku hiyohiyo  ambayo Betty alitekwa na kupotea moja kwa moja hadi wakati huo pakiwa hakuna taarifa yoyote.
Lazima kuna kitu Joy anatambua hapa!! Na ili mambo yaende sawia, lazima awe name bega kwa bega kama mpenzi wake.
Kwa kufanya hivyo nitazijua siri zote na kisha nitafaidi pesa ya Isaya!!
Alijisemea Fonga huku akirusha miguu yake huku na kule kama kwamba jambo hilo ni dogo na  litamalizika mara moja!!
Laiti angejua kisa cha Betty kutoweka, laiti angeonyeshwa japo kwa sekunde kadhaa tu mchezo ambao anataka kuingia kuucheza.
Basi angeghairisha mara moja na kuendelea na maisha yake ya kuunga-unga jijini Dar es salaam!!
Lakini Mungu ni wa ajabu, hata sekunde moja  ya mbele yako hujui nini kitatokea.
Fonga mtoto wa Manzese akajiingiza kichwa kichwa!!
Asijue kuna  nini kimejificha nyuma  ya pazia!!

*****
Betty alijaribu kuangaza huku na kule huenda atapata walau picha ya eneo ambalo alikuwa, lakini bahati mbaya hakuwa mwenyeji wa kona nyingi za jiji hilo. Hakupata hata hisia ya mahali alipo.
Na angeweza vipi kujipa uhakika kuwa yupo jijini wakati safari ya kutekwa kwake ilichukua zaidi ya masaa mawili. Huku akiwa amefungwa kitambaa usoni na bunduki shingoni iwapo ataleta usumbufu wowote ule.
Kuna muda gari lilienda kwa mwendo kasi mkubwa na kuna muda lilipunguza mwendo, kuna muda lilipita barabara yenye mabonde na kuna muda barabara ilikuwa imenyooka.
Betty alikuwa amepotezwa uelekeo kabisa, hadi alipofunguliwa tena kile kitambaa na kukutana na watu asiowajua!! Tofauti kabisa na wale waliomteka maeneoya Kinondoni wakijifanya kuwa wao ni askari polisi.
Kuna sura zilionyesha ugaidi mkubwa na zilitisha kuzitazama, lakini nyingine zilikuwa sura zilizojaa upole. Betty alitarajia kukutana na maswali mazito ambayo atashindwa kuyajibu na hatimaye kupokea kipigo kutoka kwa majangili wale. Lakini kwa siku ya kwanza aliishia kuulizwa jina lake na historia yake kwa ufupi.
Betty aliielezea kwa ufupi kweli, japo alikuwa anatetemeka!!
Alielezea alipozaliwa na anapoishi kwa sasa, alikumbuka pia kutaja elimu yake kwa uchache.
Siku zikaendelea kukatika asijue ni kipi kilichosababisha afanyiwe jambo lile. Betty akaona kukaa kimya haitakuwa na maana akaamua kuuliza.
Alimuuliza mwanaume ambaye mara kwa mara alikuwa akimpelekea chakula katika chumba alichokuwa amehifadhiwa.
“Dada, mimi sijui lolote kwa kweli yaani naishi kwa kanuni. Mimi wajibu wangu ni mambo ya usafi na chakula. Mengineyo sijui hata.” Alijibu kijana yule huku akijaribu kujitoa katika hatia.
Jibu hili likamvuruga zaidi Betty. 
Akafikia maamuzi ya kumuuliza yeyote yule ambaye atakuja mbele yake. Huenda atamfikia  muhusika  na kupata jawabu.
Kutekwa gani huku, hapigwi, hanyanyaswi wala hagombezwi na  anakula chakula kizuri tena  kwa wakati!!
Aliisubiri hiyo siku ya kuonana na mtu mwingine tofauti  na  yule muhudumu lakini haikufika upesi kama alivyotarajia.
Hadi wakati huu akijiuliza ni eneo gani la jiji la Dar es salaam anaweza kuwa yupo. Bado hakuwa na jibu la ni kwa nini amefichwa hapo? Bila kudaiwa chochote, bila kunyanyaswa!!!

****

FONGA hakutaka kulaza damu, alijipa  tahadhari kuwa alikuwa amechukua pesa ya Isaya tayari na hivyo kwa namna yoyote lazima afanye jambo la maana na  busara ili aweze kuendelea kula pesa ya kijana huyo na pia aweze kuchuma pesa zaidi.
Hakutaka kuchelerwa zaidi, akafanya mawasiliano na Joyce Kidoti. Akitaka waonane.
Joyce aliipokea simu hii kwa sauti iliyoonyesha kukata tamaa, Fonga alilitambua hilo lakini hakutaka kuuliza kupitia simu.
Kidoti akamuelekeza nyumbani kwake, Fonga akaanza safari upesi, akipitia njia za mkato ambazo zingemwezesha kufika upesi.
Majira ya saa tatu usiku alikuwa nyumbani kwa Joyce.
Walizungumza kwa kina. Joyce akihitaji pesa nyingine ya ziada lakini kwa minajiri ya kuirejesha baada ya siku tano,  Fonga naye akihitaji kujua juu ya Betty na ukombozi upi ulikuwa unahitajika aweze kuwa huru.
Joyce,alitamani sana kumpa majibu yote kama yalivyo Fonga lakini lile onyo la kutomshirikisha mtu yeyote katika mpango huo ndio lilikifanya kinywa chake kuwa kizito kusema lolote.
Akasita kumweleza Fonga juu ya masharti ya watekaji wale ambao hadi wakati huo hakuwa akiwafahamu kwa majina wala sura.
“Joyce unatakiwa ujenge imani na mimi. Uniamini name nikuamini wewe nd’o tutaweza kulitatua tatizo hili, vinginevyo litakuwia gumu sana hakika. Niambie kama kuna watu Betty ana ubaya nao labda au aliwadhulumu…eeh!!” Fonga alisihi huku akipapasa bega la Joyce.
Joyce akapinga kuwa hakuna lolote ambalo anajua kuhusu kutekwa kwa Betty lakini kuna watu anahitaji kuwapatia pesa washughulikie tatizo hilo.
“Baada ya kuona mimi nakubabaisha si nd’o hivyo Joy.” Alisema katika namna ya kusuta Fonga. Joyce akainama chini asijue namna gani anakabiliana na hali ile.
Kimya kikatanda kwa dakika kadhaa, kisha Joyce ambaye alipitiwa na mawazo mengi kwa muda akakiri katika nafsi yake kuwa alikuwa amefikwa na kama ni maji sasa yalikuwa ‘maji ya shingo’. Akaamua kutumia ule usemi wa liwalo na liwe.
Akaamua kumshirikisha Fonga juu ya jambo hili, ili walau apunguze mzigo alionao kichwani mwake.
“Fonga, sina budi kukueleza. Nakueleza kwa sababu nakuamini sana na ninajua utanisaidia, kama ulivyonitafutia pesa ile nyingi naamini hili halitakushinda, wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini hebu nikushirikishe…” alisita kuzungumza pale simu ya Fonga ilipotoa mlio wa kupokea ujumbe.
“Aah endelea..” Fonga alitaka kuupuza na kumsikiliza Joyce, lakini Joyce alimpa ishara kuwa ausome kwanza ndipo aendelee.
Fonga akatii, akaufungua ujumbe ule katika simu yake.
Baada ya kuusoma huku akiwa anaukazia macho, hapakuwa na mazungumzo tena ndani ya chumba hicho.
Mashaka yakatawala, hofu kila nukta. 
“Kuna nini kwani Fonga.” Aliuliza Joyce.
“Nitakueleza…..we nielekeze mlango mwingine wa kutokea kama inawezekana.” Aliongea sauti ya kunong’ona huku jasho likimtoka.
“Hakuna mlango zaidi ya huu!!” Joyce naye asiyejua nini kinatokea alimjibu Fonga.
Maisha ya jela, hutanua akili sana. Mara nyingi mfungwa hubuni akili zaidi ya mwenzake ilimradi tu aweze kumtawala ama la aepuke kuonewa. Mfungwa si mbumbumbu!!
Fonga aliyewahi kutumikia kifungo cha miezi tisa jela, alikuwa na mabaki ya umachachali wa jela.
Alitazama huku na kule kisha akaona chuma ngumu ambayo ilikuwa imeegemezwa katika mlango. Akaitwaa na kukimbilia chumbani kwa Joy, Joy akamfuata nyuma huku akiwa ametaharuki sana.
Akaingiza ile chuma katika nondo za dirisha la chumbani.
“wewe nyumba ya watu laki…..”
“Shhhhh!!” Fonga alimnyamazisha, huku macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa mekundu sana, jasho likimtoka lakini hakuwa na uoga tena.
Na  kwa mara ya kwanza Joyce akatambua kuwa Fonga alikuwa mtu wa mazoezi, pale alipoishuhudia misuli yake wakati akitumia chuma kile kutanua dirisha.
Nafasi ikapatikana, Fonga akamuamuru Joyce apitie dirishani, Joyce akauliza kwa nini. Fonga akamnasa kofi mgongoni nakishaakatumia amri!!
Joyce akiwa ameduwaa Fonga alimbeba juu juu na kufanikiwa kumpitisha katika tundu lile.
“Joyce,ni muda wa kuniamini mimi. Mimitu! Joyce, kuna tatizo kubwa niamini nakusihi niamini mimi.  Tumevamiwa na watu wabaya..” Fonga alimweleza kwa sauti ile ile ya kunong’ona.
“Nimeacha hela jamani……pale mezani…” Joy alilalamika huku akipiga piga miguu chini kama anayekaribia kujikojolea.
Fonga akaruka upesi, akakimbilia sebuleni. Akakwapua pochi ya Joyce.
Akarejea tena chumbani na kupita katika tundu la dirisha lililotanuliwa.  Alionekana ana mwili mkubwa lakini alitua kama paka!!!
Bila vishindo!!
Akamshika Joyce mkono , wakaanza kutoweka eneo lile.
Hawakufika mbali sana,, kikasikika kishindo.na umeme ukakatika katika nyumba aliyokuwa anaishi Joyce.
Kabla hawajashangaa zaidi ukasikika mlio wa bunduki!!!
Joyce akataka kupiga kelele, Fonga akawahi kumziba mdomo!!
“Wangeniua hawa mabwege aisee!!!” alisema Fonga kwa masikitiko!!
Joyce akabaki kuduwaa!!
Safari yao ikaishia katikanyumba ya kulala wageni!!!
Waliingia kama bibi na bwana!!
Usiku ukawakuta wakiwa wamekumbatiana!!

*****
UMAARUFU ni jambo jema na baya kwa namna moja au nyingine. Umaarufu unaweza kukuletea matatizo na wakati mwingine kukuweka mbali na tatizo.
Umaarufu mwa mtu husababisha jina lake kutamkwa na watu wengi, aidha kwa mazuri ama mabaya, kiurafiki ama kinafiki.
Hivyo ndivyo jina la Fonga lilivyotajwa na watu mbalimbali. Fonga alikuwa maarufu haswa. Wengi walilifahamu jina tu bila kuifahamu sura na bado waliweza kumzungumzia kama waliwahi kumuona.
Namba yake  ya simu ilitapakaa na kuwafikia wengi, walioitaka huduma yake waliwasiliana naye.
MALLE Stan, alikuwa mmoja kati ya watu waliowahi kusikia jina hilo na kuipata namba yake baadaye katika mazingira mengine. 
Alilisikia jina lake lilivyokuwa maarufu kisha siku aliyokutana naye akajikuta akifadhaika kukutana na mtu wa kawaida sana tofauti na jina lake. Ni siku hii aliyoamua kuchukua namba yake baada ya kuwa amefanya naye mazungumzo  ya muda mrefu kama rafiki waliyekutana kwa dharula.
Walikutana katika daladala, wakaketi siti moja. Fonga alipopigiwa simu na kujitambulisha, Malle akaanzisha urafiki akamuuliza iwapo ni yeye avumaye. Fonga hakuzungusha maneno kwa sababu alitambua fika kuwa alijulikana na wengi. Akakubali nakuendelea na stori za hapa na pale hadi kila mmoja alipofika mwisho wa safari.
Usiku huu mnene wakiwa katika kutekeleza  kazi waliyopewa na mkuu wao wa kazi. Analisikia tena jina hili la Fonga na sasa akiwa na namba yake ambayo wenzake hawakuwa nayo. 
Jina hili lilitajwa na wenzake watatu, likiwa jina geni kwao. Lakini kwake lilikuwa halina ugeni wowote. Akajiuliza je ni Fonga huyo huyo ama?
Hapakuwa na sifa yoyote mbaya katika jina hili, na mbaya zaidi kumfahamu kabla ya tukio hilo kukamweka katika hatia ya kujiona akijihusisha katika mauaji ya mtu ambaye anamfahamu.
Malle, hakuwa tayari na hakuwahi kuua mtu anayemfahamu walau kwa jina tu. Kwa matukio haya ili asiyakumbuke alikuwa tayari kuua asiowafahamu mia kuliko mmoja anayemfahamu.
Hali hii iliathiri sana ubongo wake!!
Alijua kuwa wakifanikiwa kuingia katika nyumba ile isiyokuwa na mlinzi basi hataweza tena kumtetea Fonga. Wakati ulikuwa ni  ule. 
“Roho yake ipo mikononi mwangu!!” Malle alijisemea.
Akachukua simu yake akautuma ujumbe  mfupi wa maandishi kwenda katika namba ya Fonga!! Namba aliyopewa siku ile katika gari!!
“Kama upo na Joyce, ondoka naye fasta. Kuna wajinga wanaitaka roho yako usiku huu kisha wanaondoka na Joyce. Fasta….” Ujumbe ukatumwa!!!
Ni ujumbe huu uliomkurupua Fonga na kufanikiwa kutoroka asijue aliyemuokoa ni nani….
Malle  akiungana na wenzake watatu waliivamia nyumba ile  katika hali ya kishari shari kama walivyokubaliana. Malle hakuwa na imani kuwa ujumbe ule umesomwa na Fonga huyu anayetaka kuuawa usiku huu ama la! 
Lakini kitendo cha kuikuta nyumba tupu, kisha walipoingia chumbani wakakuta nondo imetanuliwa.
Malle akakiri katika nafsi yake kuwa Fonga ni zaidi ya anavyomfikiria!!! Hakutarajia angekuwa mwepei kiasi hicho.
Majambazi wengine nao wakakiri kuwa.
Fonga alikuwa kiboko!!!
Hawakujua kuwa mwenzao mmoja aliwazunguka.
Wakatoweka baada ya dakika kumi za kutikisa mtaa!!

Asubuhi na mapema walikuwa mbele ya meza ya kung’ara ya Mzee Beka.
“Sijaona kichwa cha habari hata kimoja juu ya kifo chake!!”  Beka aliunguruma huku akizunguka katika kiti chake.
“Bwege kapitia dirishani aisee…sijui kashtukaje tu” alijibu kiongozi wao.
“Yeye nd’o bwege ama nyie aliyewatoroka? mnamuita bwege, yaani anapita na yule Malaya wake dirishani mnasema bwege. Bastard!!!” aling’aka huku akitabasamu, vijana wale wakatambua kuwa amechukizwa na kilichotokea. Kila alipokasirika alikuwa akitabasamu.
Hawakuwa na cha kujibu!!!
“Sihitaji maelezo marefu zaidi. Sitanunua gazeti lolote hadi mtakaponiletea gazeti likizungumzia kifo cha Fonga!!” aliamrisha kisha akafanya ishara ya kuwafukuza vijana wale!!
“Na sihitaji kukaa wiki nzima bila kusoma magazeti….” Alimalizia huku na wao wakimalizia kutoka nje ya ofisi ile.
Beka akisema huwa anamaanisha!! 
Hilo walilitambua, kila mmoja akaondoka na lake kichwani akijaribu kutafakari ni namna gani watamridhisha Beka. Kasoro Malle tu!! 
Yeye aliwaza juu ya Fonga!!

***FONGA anasakwa auwawe……nani anamsaka na kwa nini??
**Kwanini Fonga alitakiwa kuuwawa kisha Joyce abaki hai??
***Betty naye hajui alipo na kwa nini ametekwa..
***ISAYA anangoja majibu ya Fonga…
**Mzee Beka ni nani katika mpango huu…na kwa nini??

**ITAENDELEA…..
#Asanteni kwa maombi yenu….naendelea vizuri kiasi japo sijawa imara…..

ROHO MKONONI

Post a Comment

Previous Post Next Post