Mwanaume mmoja raia wa Afrika Kusini amejikuta akinyimwa Viza ya kuishi nchini New Zealand kutokana na kuwa mnene wa kupitiliza.
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC maafisa wa utawala nchini New Zealand
wamemwambia mwanamume huyo aitwaye Albert Buitenhuis ambaye pia ni
mpishi kuwa ni mnene kupita kiasi kuweza kuruhusiwa kuishi nchini humo.
Maafisa hao walisema kuwa Buitenhuis, mwenye uzito wa kilo 130 hana afya
nzuri.
Bwana Buitenhuis na mkewe walihamia nchini New Zealand mwaka (2007).
Wakati huo mwanamume huyo alikuwa na uzito wa kilo 160 kiasi ambacho
amefanikiwa kupunguza kilo 30 na kuwa 130 ambazo hata hivyo bado
haijamsaidia kuruhusiwa kuendelea kuishi nchini humo.
Albert na mkewe
“Tumekuwa tukiomba viza hizo kila mwaka na hapajawahi kuwa na
matatizo yoyote,hawajawahi kuzungumzia uzito wa Albert wala afya yake
wakati hata alipokuwa mnene kushinda sasa.”alisema mke wa Albert.
Lakini mapema mwezi Mei, wanandoa hao waliambiwa kuwa hawatapokea visa mpya kwa sababu ya unene wa bwana Buitenhuis.
“nimeshangazwa sana kwa sababu kwa sasa ameweza kupoteza kilo 30 tangu tuje hapa New Zealand, ” alisema mkewe Buitenhuis.
Wawili hao wamemuomba waziri wa uhamiaji wa nchi hiyo kuwaruhusu
waendelee kuishi nchini humo kwani bwana Buitenhuis ameweza kupoteza
kilo.
Msemaji wa uhamiaji alisema kuwa bwana Buitenhuis alinyimwa visa mpya
kwa sababu ya tisho kwa afya yake kutokana na uzani wake, kuwa anaweza
kupatwa na kisukari, shinikizo la damu na maradhi ya moyo.
New Zealand ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wenye unene
kupita kiasi huku takriban asilimia 30 ya watu wake wakiwa waathiriwa.
SOURCE: BBC
Post a Comment