Bingwa wa Wimbledon Andy Murray
ameshindwa kwa mara ya kwanza tangu mwezi wa Mei wakati alilpopambana na
Ernests Gulbis katika raundi ya tatu ya kombe la Rogers Cup mjini
Montreal.
Gulbis raia wa Latvia, anashika nafasi ya 38
katika orodha ya wachezaji bora duniani,alishinda kwa seti mbili mbili
kwa mfulululizo matokeo ya 6-4 6-3 .Murray alisema hapana shaka ana kazi kubwa ya kufanya kabla ya mashindano ya ubingwa wa Marekani.
Mashindano hayo ya Montreal ni ya kwanza kwa Murray tangu ashinde ubingwa wa Wimbledon mwezi uliopita .
Murray, ameshawahi kushinda mara mbili nchini Canada lakini safari hii Gulbis alimkatiza katika safari yake ya kunyakua ubingwa, Hii ni mara ya kwanza kwa Gubis kumshinda Murray katika mechi sita walizokutana.
Awali wapinzani wakubwa wa Murray,Rafael Nadal na Novak Djokovic walishinda mapambano yao. .
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24 Canada imewakilishwa katika robo fainali na wachezaji wawili Vasek Pospisi na Milos Raonic.
Post a Comment