Washiriki
wa ‘The Chase’ mchana huu wamepata ugeni wa kushtukiza wa rapper Ice
Prince kutoka Nigeria ambaye ametia timu katika jumba la Big Brother
kama balozi wa One Campaign na kupiga story na housemates wanaoendelea
kuzi chase $300,000 za Biggie.
Washiriki wa Ruby walishindwa kuzuia furaha zao mara baada ya kumuona
star huyo aliyeingia mjengoni kwa style ya aina yake bila taarifa.
Ice Prince ambaye ametembelea nyumba ya Big brother kama balozi wa
One Campaign kwa kushirikiana na African Union, ametumia uwepo wake
katika nyumba hiyo kuchat na washiriki pamoja na kuwahamasisha
kujihusisha na huduma za kijamii hata wakiwa nje ya Big Brother
watakapokuwa wamerejea katika nchi zao.
Ice Prince ambaye jina lake halisi ni Panshak Zamani, ameendelea
kuwaeleza washiriki kuwa sasa wamekuwa mastaa nje ya mjengo hivyo
wajitahidi kutumia ukubwa wa majina yao kwa faida ya jamii.
“Whether you win the money or not you guys should get involved,
hopefully by 2030 extreme poverty should be eradicated. Your voices and
your images will do that in a lot of ways”. Alisema Ice Prince
Post a Comment