UONGOZI
wa Boom FC umelishukuru Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
kwa kuipatia msaada wa Sh 5,125,000 kwa ajili ya uendeshaji wa timu hiyo
katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Boom FC, Duni Mibavu amesema
fedha hizo zitasaidia timu kufanya vizuri katika ligi na kuwapa morali
wachezaji ili kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu
ujao.
“Tunawashukuru
wenzetu wa NSSF chini ya Mkurugenzi wake Dk. Ramadhan Dau kwa msaada
mkubwa walioutupatia, hii inaonyesha ni jinsi gani walivyoguswa na na
kilio chetu na kuamua kutusaidia ili tufanye vizuri,” alisema.
Duni
ameomba na mashirika mengine pamoja na makampuni mbalimbali nayo kuiga
mfano wa NSSF katika kuzisaidia timu za madaraja ya chini ili nazo
zifanye vizuri.
Post a Comment