China na Afrika kulipana kibiashara kwa kutumia sarafu ya China RMB

 
Mkurugenzi wa benki ya Benki ya China tawi la Afrika Kusini Qiu Zhikun amesema, sarafu ya China Renmibi itatarajiwa kutumika katika malipo ya biashara kati ya China na bara la Afrika.

Amesema hiyo inatokana na kuongezekwa kwa biashara kati ya pande hizo mbili. Mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 200, na thamani ya biashara kati ya China na Afrika Kusini ilifikia dola za kimarekani bilioni 60.

Katika miaka minne iliyopita, benki hiyo imefungua akaunti 1,000 za RMB kwenye nchi zaidi ya 80, hivyo kuanzisha mtandao unaotumia RMB sehemu mbalimbali duniani. (Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa)

Post a Comment

Previous Post Next Post