Cristiano
Ronaldo amesaini mkataba mpya utaomfanya aichezee Real Madrid hadi
mwaka 2018 mkataba ambao unamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi
zaidi nchini Hispania kwa kupokea kiasi cha Euro milioni 17 kwa mwaka
pamoja na kupewa haki ya 60% ya matangazo na zinazo baki zitaenda Real
Madrid.
Hata hivyo, sasa ataongeza asilimia hizo, japokuwa klabu nayo imebaki
na haki zake pamoja na kuhakikishiwa kupata faida za kiuchumi kutoka
kwa uwekezaji utaofanywa kutokana na kutumika kwa fedha
zitakazotengenezwa na matangazo ya Cristiano Ronaldo.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez na Cristiano Ronaldo walikuwa
na majadiliano ya muda mrefu, lakini hatimaye wakafikia mwisho kwa
maelewano na kufuta tofauti zao zilizokuwa msimu uliopita.
“Kila kitu kipo sawa kwa sasa, wamekuwa na maelewano mazuri,” walisema watu wa karibu wa pande zote mbili.
Real Madrid imepanga kutangaza mkataba huo mpya na Ronaldo kabla ya
kuanza kwa ligi hapo Agosti 17 ingawa inaonyesha mkataba huo mpya si
kwa sababu ya fedha pekee, lakini ni mapenzi pia na kwasasa atapata
ulinzi wa rais wa klabu , klabu yenyewe, wachezaji wenzake pamoja na
mashabiki ,kwamujibu wa chanzo hicho cha habari.
Florentino anataka kuhakikisha Cristiano Ronaldo anabaki Real Madrid
hadi atakapostaafu kama ilivyokuwa kwa Jorge Mendes, ambaye sasa ni
wakala wa wachezaji.
Ni Mendes ambaye alifanikiwa kumshawishi Cristiano Ronaldo kukubali
kuondoka katika klabu hiyo kwa sababu hakuna klabu bora duniani zaidi ya
Real Madrid. Hata hivyo, Samuel Eto’o amebaki kuwa ndiye mchezaji
anayelipwa zaidi duniani kwa sasa akifuatiwa na Ronaldo anayeongoza kwa
Hispania pamoja na Messi.

Post a Comment