D'BANJ NA DON JAZZY" WAUNGANA TENA BAADA YA KUSAMBARATIKA MWAKA JANA!

Don-Jazzy-DBanj
Kama mnavyo kumbuka mnamo mwezi March mwaka 2012 mwanamuziki maarufu wa Nigeria D'BANJ
alitengana na Mwenzie DON JAZZY baada ya kupishana jinsi ya mwelekeo wa group lao hilo.Kutokana
na jinsi ugomvi ulivyo kuwa mkubwa hawajawahi kuonekana pamoja tena toka mwezi huo wa March wala haijawahi kusikika kuwa wanamuziki hao huwa wana mawasiliano hata ya simu.
        Jambo lilowashangaza wenzi Juzi kati kwenye sherehe ya Harusi ya dada yake D'BANJ ..DON JAZZY na D'BANJ wamepanda jukwaa moja kwa pamoja nakuwatumbuiza waarikwa zile nyimob zao zilizo hit wakati wakiwa pamoja.Kitendo hicho kiliwashangaza wengi kwani hawajawahi kuonekana hata wakiongea toka walipo sambaratika.
       Mwandishi wetu wa burudani "DMK" alipozungumza na watu wachache washabiki wa group hilo walionekana kufurahia sana kitendo hicho nakuomba kuwa warudi pamoja kama group kutoa ngoma zingine kwani vipaji vyao vikiungana hawana mpinzani ....wengine walisema hata P'SQUARE hawawafikii ...je ni kweli???...Angalia Video wakiburudisha pamoja.
 
 

Post a Comment

Previous Post Next Post