Feza Kessy aingia tena kwenye kikaango cha Eviction, aongoza kwa kutajwa mara 4

374442_500432656704965_690117850_nWakati ambapo hajamaliza hata saa 24 tangu panga la eviction limpitie mpenzi wake Oneal, Feza Kessy ameongoza kwa kuwa na nominations 4 za kutoka wiki hii. Hiyo inamaanisha nini? Inaamanisha kuwa Feza anahitaji kura za Afrika Mashariki kumwokoa asitoke. Ikumbukwe kuwa Feza aliponea chupu chupu kutoka jana kwakuwa Nando aliondolewa wiki iliyopita kabla ya jana lasivyo naye angekuwa nyumbani sasa. Atasurvive awamu hii?
Ugumu unakuja kwakuwa Bimp naye atakuwepo kwenye list ya watakaopigiwa kura za kuokolewa. Ametajwa mara tatu na Cleo pia akiwa na kura tatu. Bimp anaonekana kuwa kipenzi cha Afrika kwa sasa hasa kwakuwa jana aliokolewa na nchi 10.
Mkuu wa nyumba, HoH, Mnaijeria Beverly atamuokoa nani? Tuombe Mungu amhurumie Feza.
Hivi ndivyo nomimations zilikuwa:
Bimp: Elikem and Dillish
Elikem: Bimp and Feza
Cleo: Feza and Beverly
Feza: Elikem and Cleo
Melvin: Beverly and Feza
Dillish: Feza and Bimp
Angelo: Cleo and Bimp
Beverly: Cleo and Dillsih

Post a Comment

Previous Post Next Post