Rais
wa zamani wa Marekani George W. Bush jana alilazimika kufanyiwa
operation ya moyo huko Dallas, Texas Marekani baada ya madaktari
kugundua mishipa ya damu iliyokuwa imeziba katika moyo ‘an artery
blockage’.
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya Bush Freddy Ford , baada ya
madaktari wa Cooper Clinic kugundua tatizo hilo wakati wa checkup yake
ya kawaida Jumatatu wiki hii, walimshauri Bush afanyiwe upasuaji, zoezi
lililofanyika Jumanne (August 6) katika hospitali ya Texas Health
Presbyterian.
Katika taarifa hiyo Ford aliendelea kusema operation hiyo ilimalizika
salama na sasa Mr Bush yuko katika hali nzuri kiasi cha kumfanya
atamani kurejea nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kila siku,
“President Bush is in high spirits, eager to return home tomorrow and
resume his normal schedule on Thursday,”.
Mr Bush mwenye miaka 67 amewahimiza watu wajiwekee utaratibu wa
kupima afya zao mara kwa mara sababu tatizo kama lake limegundulika
wakati wa checkup yake ya kawaida.
Bush anategemewa kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano na kesho ataendelea na shughuli zake.
SOURCE: REUTERS
Post a Comment