Afisaa mmoja wa chama cha
kitaifa cha wafanyakazi wa migodini (NUM) ameuawa kwa kupigwa risasi
katika mgodi wa madini wa Marikana nchini Afrika Kusini ambako wachimba
migodi wengine 34 waliuawa na polisi mwaka mmoja uliopita.
Wanachama wenzake wamesema kuwa mwanamke huyo ambaye ni muuza duka aliuawa asubuhi ya leo.Uhasama kati ya vyama vya wafanyakazi, katika mgodi huo umesababisha kuuawa kwa wafanyakazi kadhaa katika mwaka mmoja uliopita.
Haijulikani ikiwa mauaji ya leo yanahusishwa na mzozo uliopo sasa kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi.
Chama cha NUM kimesema kuwa kimekasirishwa na polisi kutopiga hatua katika kuwakamata wahusika kwa kile walichosema ni mauaji ya kupangwa katika mgodi wa Marikana.
Msemaji wa Lonmin, Sue Vey, aliambia shirika la Reuters kuwa polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza mauaji hayo.
Mauaji yaliyotokea mwaka jana mwezi Agosti yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Afrika Kusini kupata uhuru
Post a Comment