Lucy Komba
Muigizaji maarufu Swahiliwood Lucy Komba amesainishwa mkataba wa kufanya kazi zake za
filamu na kampuni ya nchini Denmark inayoitwa Twaleb Entertainment ambayo
inamilikiwa na Abou Hermis Twaleb mtanzania anayeishi nchini humo kwa takribani
miaka 12 sasa tangu mwaka 2001. Akizungumza exclusively na Swahiliworldplanet
juzi Twaleb alisema "kwa kifupi ni kwamba Lucy Komba ameshaingia mkataba
na Twaleb Entertainment ambayo mimi ndio mmiliki. Nimefurahi sana kuwa karibu
na Lucy na kwa kuwa namkubali sana kikazi katika tasnia ya filamu na hakuna
atakayepinga ninachokisema. Na kwa upande mwengine ni mtu muhimu sana tofauti
na baadhi ya mastaa wengine kwa kuwa uwezo wake ni mkubwa kiasi cha kunifanya
niwe navutiwa sana na uchapaji kazi wake kwa kuwa yeye ni kila kitu
nikimaanisha ni actreess, producer, director na pia ni writer mzuri sana wa
story . Na ndiyo sababu nimeamuwa kufanya naye kazi ingawa tayari wapo wasanii
wengi wengine ambao tayari wameshawasiliana na mimi kuhusu kuja kufanya kazi na
mimi katika siku zijazo". Soma zaidi
Kampuni
hiyo inaanza kutengeneza filamu yake ya kwanza mwezi huu wa nane huku Lucy
Komba akiwa mmoja wa waigizaji wakuu "Utengenezaji wa film yangu ya kwanza
unaanza mwezi huu huu baadaye na Lucy Atashiriki, kuhusu Jina la movie hiyo na
washiriki wengine wa movie hiyo nitayatoa maelezo hayo baadaye" alisema
Twaleb. Aliendelea kwa kuongeza kuwa nia na malengo ya kampuni hiyi ni
kuzitangaza filamu za kitanzania na pia kuindeleza na kuzidi kuitangaza lugha
ya kiswahili ambayo tayari inazungumzwa na mataifa mbalimbali na ikisemekana
kuwa moja ya lugha rahisi kujifunza. "Madhumuni ya (TE) Twaleb
Entertainment ni kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu haswa kukitangaza
Kiswahili katika hatua ya juu na pia kuweza kuutangaza utamaduni na desturi
zetu ili ulimwengu ujue zaidi kuhusu Tanzania na lugha hii ya Kiswahili"
Pia
alisema malengo ya Kampuni hiyo ni kufanya kazi Denmark na Tanzania na pia
kuwatumia wasanii wengine katika kuendeleza vipaji vyao na kampuni hiyo
itafanya kazi na msanii yoyote yule mwenye sifa " Nitakuwa nashirikisha
wasanii mbalimbali na nitakuwa nafanya kazi hapa Denmark na pia Tanzania. Na
lengo langu kubwa ni kuinua wale wenye vipaji ambao kwa njia moja au nyingine
hushindwa kujiendeleza, Twaleb Entertainment ni ya wote. Soma zaidi.
Twaleb na
Lucy wakiwa katika pose la picha ya pamoja
Filamu za
kampuni hiyo zitasambazwa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania "Filamu zote
zitakazokuwa zinatengenezwa na TE zitakuwa zikiuzwa katika nchi tofauti
ikiwezmo Tanzania kama sehemu kubwa kiusambazaji lakini niko kwenye mipango ya
kusambaza movie katika nchi yoyote ile ambayo nitakuwa na mwakilishi. Alisema
pia filamu za kiswahili zinapendwa sana Denmark na soko lipo na mikakati ya
filamu za kampuni hiyo ni kuinia katika soko la nchi zote jirani na Denmark
yaani Norway, Germany na Sweden ambazo ni nchi zenye ushirikiano wa karibu na
Tanzania.
Lucy Komba
ni muigizaji wa siku nyingi ambaye licha ya kujaaliwa kipaji na kuwainua
chipukizi wengi wa filamu nchini lakini kwa muda mrefu amekuwa akifanya juhudi
katika kutangaza filamu za Kiswahili nchi mbalimbali na ameshatokea kwennye
media kadhaa za nje ya nchi katika juhudi zake hizo kwa hiyo filamu mpya za
Twaleb Entertainment na Lucy Komba sio za kukosa kwa wapenzi wa filamu za
kiswahili. Pia sio mara ya kwanza kwa muigizaji huyo kucheza filamu nchini
kwani tayari kuna filamu ameshacheza na wasanii wengine nchini Denmark
Post a Comment