Maadhimisho ya miaka 50 ya March in Washington


 
Picture
Picture
Angela Bassett Evelyn katika flash ya swahilivilla pale ilipomnasa alipokuwa akisubiri gari lake kufanyiwa upekuzi wa lazima kabla ya kuingia eneo la tukio
Picture
Picture
Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani Forest akishangaa kwa mbali flash ya "swahilivilla blog" baada ya kutolewa ndani ya gari lake na kufanyiwa utaratibu wa kupekuliwa kabla ya tukeo kuanza rasmi.
Jana, Agosti 28, 2013 Wamarekani waliadhimisha rasmi miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano makubwa ya kudai haki sawa kwa "watu weusi" nchini humo.

Katika maadhimisho hayo, kamera ya "swahilivilla blog" iliegeshwa kando ya lango la kuingia na kushuhudia watu maarufu nchini wakipekuliwa kwa sababu za usalama kabla ya kuingia ndani sherehe hizo ambazo zilihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini.


Picha hizo zinaonekana hapo juu na hapa chini pamoja na sauti...
Tuliobahatika kuwanasa katika kamera ya swahilivilla muigizaji Jimmy Foxx, pale alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial Washington DC. Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)

Muigizaji wa filamu Jimmy Foxx akishuhudia gari lake likipekuliwa kabla ya kuingia ndani ya tukio la maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC

Mwigizaji wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial Washington DC

Mshangao mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani John F. Kennedy, Caroline Kennedy ambae ni balozi mteule Nchini Japani, alipoingia na Cab (Taxi). cha kuchangaza pia ni pale gari lake lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.

Caroline Kennedy akiishangaa flash yaswahilivilla blog pale ilipomnasa akisubiri gari lake likifanyiwa upekuzi wa lazima

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani Forest naye pia gari lake lilifanyiwa upekuzi na maofisa wa usalama baada ya kuwasili katika endeo la Sherehe za miaka 50 ya March on Washington DC

Vile vile kamera ya swahilivilla blog imemnasa Rajiv “Raj” Shah American Economic development specialist, alipotolewa nje ya gari lake na kufanyiwa upekuzi wa lazima siku ya Jumatano Aug 28, 2013 Washington DC

Rajiv “Raj” Shah akishangaa kwambalii flash ya swahilivilla.blog baada yakutolewa ndani ya gari lake na kufanyiwa utaratibu wa kupekuliwa.

Ofisa Usalama akifanya upekuzi wa magari ya watu maarufu yanayoelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC siku ya jumatano Aug 28.

Mwanasheria Mkuu wa jimbo la California Kamala Harris pia alishushwa ili kuruhusu upekuzi wa gari kabla ya kuingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington

Kamala Harris aliamua kusogea na kusalimiana na baadhi ya watu waliokua karibu yake pamoja na kamera ya swahilivilla wakati gari yake ikipekuliwa kabla ya kuingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington

Ni Oprah Gail Winfrey pekee ambaye hajatoka kwenye gari lake ambalo lilipekuliwa na kuruhusiwa kuondoka bila ya kutolewa ndani ya gari hilo alilokua amalipanda

Oprah Gail Winfrey akishangaa kwa mbali flash ya swahilivilla wakati anaelekeaa ndani ya Lincoln Memorial Washington Washington DC 

Chief wa swahilivilla Abou Shatry akiwa katika 50th anniversary March on Washington DC Siku ya Jumatano 28, 2013 Rais Barak Obama, leo ametoa changamoto kwa kizazi kilichopo kuwaenzi mashujaa walioandamana mwaka 1963 kudai haki sawa kwa watu wa rangi zote nchini Marekani. JAMII RADIO ina ripoti kamili. Sikiliza. Na pia kwa taswira zaidi bofya hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post