Mahakama kutoa uamuzi kuhusu uchaguzi-Ghana

Rais Mahama
Mahakama ya rufaa nchini Ghana, inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi iliyowasilisha mbele yake kupinga ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi mkuu uliopita.
Chama cha NPP, kimedai kuwa ushindi huo haukuwa halali madai ambayo yamepingwa vikali na chama tawala wa NDC.
Kesi hiyo imekuwa ikionyeshwa moja kwa moja katika runinga ya taifa, hali inayoashiria uwazi wa idara ya mahakama nchini humo.
Kwa miaka nyingi Ghana imeonekana kuwa mfano mzuri wa utawala wa demokrasia barani Afrika.
Takriban maafisa elfu thelathini wa ulinzi wametumwa katika maeneo kadhaa ili kuzuia ghasia, baada ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake.
Mahama, wa chama cha National Democratic Congress (NDC), alishinda uchaguzi wa urais decemba mwaka uliopita kwa kuzoa asilimia hamsini nukta saba ya kura zote naye mpinzani wake, Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic Party (NPP) akipata asilimia 47.
Uchaguzi huo uliendeshwa kwa njia ya amani na rais Mahama na mpinzani wake Akufo-Addo wamehaidi kuheshimu uamuzi utakaotolewa na mahakama.
Mahama aliapishwa rasmi Januari mwaka huu.
Raia wa nchi hiyo wamekuwa wakifuatilia kesi hiyo ambayo imekuwa ikionyeshwa katika runinga na kupeperushwa na radio ya taifa.
Chama cha NPP kimeomba mahakama kufutilia mbali hesabu ya zaidi ya kura milioni nne, kikisema matokeo yalivurugwa ili kumhakikishia ushindi Bwana Mahama katika raundi ya Kwanza.
Lakini chama cha NDC nacho kinasema makosa yaliyofanywa na maafisa wa tume ya uchaguzi wakati wa kuhesabu kura sio njama ya kuhujumu demokrasia na kuwa hakunan sababu yoyote ya maana kwa mahakama hiyo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo wa Urais.
- BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post