Majambazi waliovaa sare za polisi waivamia Habib Afriican Bank ya Dar na kuiba mamilioni


kko
Kariakoo
Taarifa kutoka kituo cha runinga cha ITV zinasema watu wasiofahamika leo wamevamia benki ya Habib Afriican (Bank) iliyoko Kariakoo, jijini Dar es salaam na kupora mamilioni ya fedha.


Hii ni taarifa iliyoandikwa katika mtandao wa kituo hicho:
Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha. Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Ripota wa kituo hicho Sam Mahela aliyekuwa akiripoti kutoka eneo la tukio muda mfupi uliopita kupitia ITV, amesema mashuhuda wamesema majambazi hao walikuja na gari aina ya Noah huku mmoja wao akiwa amevaa sare za jeshi la polisi.
SOURCE: ITV

Post a Comment

Previous Post Next Post