Milliband kupinga Uingereza kuishambulia Syria

Ed Miliband
Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Labour, nchini Uingereza, Ed Miliband, amesema bunge la nchi hiyo halipaswi kuamua ikiwa itaidhinisha mzozo wa Syria kutatuliwa Kijeshi.
Milliband ameyasema hayo muda mfupi kabla ya bunge la Uingereza kupiga kura ikiwa Uingereza itaishambulia Syria, kufuatia madai ya kutumia silaha za kemikali mjini Damascus.
Waandishi wa habari wanasems serikali ya Uingereza inahofia huenda ikapoteza kura hiyo na hivyo kukosa idhini ya kuingilia mzozo huo wa Syria.
Milliband amesema wamejifunza mengi kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa miaka ya zamani kama ule wa kuivamia Iraq.
Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuipa jopo maalum na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nafasi ya kufanya kazi yao.
Serikali ya Uingereza imesema ina habari za kujasusi kuhusu Syria na itachapisha ripoti hiyo na ushauri wa kisheria kabla ya mjadala huo kuanza bungeni.
- Bbc

Post a Comment

Previous Post Next Post