Mkulima mmoja mkoani Singida auawa kwa kukatwakatwa baada ya kudhaniwa kuwa na fedha za mauzo ya mazao.


DSC02443
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa ya mauaji ya mkulima mkazi wa kijiji cha Mkuru tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba, Said Juma ambaye pia aliporwa shilingi 250,000 na majambazi hayo.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mkulima mkazi wa kijiji cha Mkuru tarafa ya Ndago wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Said Juma (32), amefariki dunia baada ya kukatwa katwa kwa mapanga na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea Agosti 7 mwaka huu saa saba usiku hulo katika kijiji cha Mkuru.
Amesema watu hao walimwambia Said (marehemu) kuwa wanazo taarifa kwamba ameuza mazao na hivyo wanazihitaji fedha zote za mauzo ya mazao.
Kamanda Kamwela amesema “Said alipodai kuwa hana fedha na kwamba hajauza mazao yoyote, walianza kumkata kata kwa mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake papo hapo.
Baada ya kutimiza azma yao hiyo, wakipora shilingi 250,000 za marehemu na kukimbilia kusiko julikana”.
Amesema kwa sasa wanamshikilia Athumani Dotto (36), Chinko Shaban (29) na Kisiku Juma (28) wote wakazi wa kijiji cha Mkingi.
Upelelezi ukikamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji na uporaji wa shilingi 250,000

Post a Comment

Previous Post Next Post