MAREHEMU RESTUTA MAYUMA
Ni
masikitiko makubwa kwa wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)
kampasi ya Dodoma kwa kumpoteza mwanafunzi mwenzao Bi. Restuta Mayuma
ambaye alifariki tarehe 05/08/2013 (Jumatatu) mnamo mishale ya saa kumi
na moja jioni.
Hata
hivyo mwanafunzi huyo alikuja dodoma kwa lengo la kufaya mitihani yake
( katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wa Chuo cha CBE wamekuwa
wakiendelea kufanya mitihani yao ya Special pamoja na ile ya
Supplimentary.
Marehemu
Restuta, Alikuwa anasoma Diploma , kozi ya Uhasibu (Accountancy) ,
ambapo alianza masomo ya Diploma mwaka wa masomo 2011/2012 na alitakiwa
kuhitimu Elimu yake ya Diploma mwaka 2012/213.Lakini kwa kipindi
hiki alikuja chuo kurudia mitihani yake ya Diploma I .
Akizungumza
na blog hii Rafiki wa karibu sana na Mwanafunzi huyo
(Marehemu Restuta) alisema Marehemu alikuwa anasumbuliwa na homa za
hapa na pale (Malaria) hali ambayo ilipelekea mpaka kutokea kwa kifo
chake.
Tayari
Mwili wake umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Dar es salaam eneo la
BUNJU kwa ajili ya shughuli za Mazishi ambapo mwili huo umesafirishwa
na Gari la Chuo (CBE) Kwa kuambatana na WARDEN, Mashauri Machunde
(Mwanafunzi CBE) pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu waliokuwepo
mkoani Dodoma.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Bw. Mashauri Machunde (Mwanafunzi CBE) amewataka
wanafunzi wote wa CBE wanaoishi jijini Dar es salaam kijitokeza katika
mazishi ya Mwanafunzi huyo yanayotarajiwa kufanyika kesho nyumbani
kwao "Bunju " Kwa kupanda magari yaendayo Bunju na kushukia eneo la
Bunju "A" kituo kinaitwa Shule au Hospital (Uliza kwa Mzee Mayuma karibu na Shule ya Sekondari Fanaka)
Mpaka
tunarusha habari hii hewani bado muda wa mazishi haujafahamika
(Endelea kutembelea Blog hii kwa ajili ya kupata Habari zaidi juu ya
msiba huo).
"Hii ni safari ya kila mmoja , Mwenzetu katangulia . Kwa masikitiko
makubwa Mmiliki wa Blog hii Mr Boss Ngasa anatoa pole kwa
Familia na ndugu jamaa na Marafiki waliofikwa na Msiba huo"
NOTE:
Kwa wote walioko Dar es salaam waweza kuwasiliana na Mashauri Machunde kwa namba : 0652-559011 ili kufika eneo la msiba (BUNJU)
Credit:na Dodoma university
Post a Comment