Rapper
Hamidu Chambuso aka Nyandu Tozi, ambaye yupo kwenye maandalizi ya
kufanya video ya wimbo wake, Kwa Mafans amesema hali ya muziki ilivyo
nchini ilimfanya ajiongezee kufanya mishemishe zingine zinazomweka mjini
kwa sasa.
“Kuna wakati nilifanya muziki kama maisha haikuwa kama nilivyotegemea
nikaona nifanye misheni town pamoja na ujasiriamali na muziki nifanye
kama burudani kwa fans wangu na mimi mwenyewe kwasababu muziki upo
kwenye damu,” ameongea “Kwangu mimi nategemea muziki 30% na
zilizobaki nafanya misheni town pamoja na ujasiriamali.”
Rapper huyo amewashauri wasanii ambao muziki hauwaendei vizuri, kuwa wajishughulishe na mambo mengine tofauti.
“Kama muziki umebana usishindane na game utakuwa kichaa fanya muziki
kimaslahi kama haulipi fanya mipango mingine na muziki fanya kama
burudani,”amesisitiza.

Post a Comment