Rais Jakaya Kikwete ametembelea raia wawili wa uingereza waliolazwa katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam baada ya Kumwagiwa tindikali

Rais Jakaya Kikwete ametembelea raia wawili wa uingereza waliolazwa katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam baada ya Kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana huko visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam baada ya kuwatembelea raia hao wawili ambao ni Katie Gee na mwenzake Krist Trup wenye umri wa miaka 18 kila mmoja,rais Kikwete amesema ameskitishwa na tukio hilo na kwamba wakati wanaendelea kupewa matibabu vyombo vya usalama vinaendelea kufanya kazi yake ili kubaini waliohusika na tukio hilo ambalo Mh rais amesema ni tukio la aibu

Mwenyeji wa wagonjwa hao waliomwagiwa na tindikali na watu wasiojulikana,Bwana Bashir Ismael kutoka visiwani zanzibar,amesema raia hao walilkuja hapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufundisha na kwamba ni walimu wa shule ya St Monica inayomilikiwa na moja ya taasisi za dini ya kikiristo ambalo lipo eneo la mkunazini stone town.

Baada ya mh rais kuwatembelea wagonjwa hao,alipita katika chumba kingine kumjulia hali mbunge wa jimbo la bariadi Mh John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali hiyo ya Aga Khan kutokana na tatizo la shinikizo la damu ambapo kwa mujibu wa mpwa wa mbunge huyo aliyejitambulisha kwa jina la Bwana Wanjoda Mwinamila,amesema Mh Cheyo anaendelea vizuri

source:;ITV

Post a Comment

Previous Post Next Post