Kipande
cha mwisho cha kipindi cha The Interview cha Clouds TV ambapo
kilihusisha mahojiano na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C
kilirushwa jana usiku.
Katika sehemu hiyo Ray C alizungumzia jinsi ilivyokuwa ngumu kwake
kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, wasanii wengi walivyoingia
kwenye janga hilo na jinsi Tanzania ilivyoathirika na madawa hayo.
“Hali ni mbaya, wasanii wengi, wengi sana wameingia, sitaki kujua
wameingiaje lakini najua kama nilivyoingizwa nao wameingizwa hivyo.
Kwamba wasanii ‘aah anaimba tu pale anapata milioni tano, yaani msanii
hana kazi anapiga piga tu yoyoyo, kashapata pesa. Kwahiyo pesa zao si za
mwisho wa mwezi, lisaa limoja kaimba kashapata pesa. Kwahiyo wanafuatwa
wale, tuwaingizie ili na wao wakishakuwa maaddict pesa zao zote
wanazopata tutazipata sisi. Kwahiyo usishangae wasanii wengi wameingia
lakini najua wameingizwaje, kwa style hiyo. Kwahiyo ni wengi sana sasa
hivi, si wa filamu, si wanamuziki,” alisema.
“Addiction si kwa wasanii tu. Kuna watu wanakuja na tai nzuri
anaonekana yeye anafanya kazi benki kumbe akitoka hapo anaenda anapona
halafu anarudi. Kwahiyo ni kila Mtanzania yeyote, Watanzania tumeumia,”
alisisitiza.
“Si watoto wa shule, si wasanii, si watu wazima na tai zao. Huu ni
ugonjwa, ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine. Addiction is a disease like
any other disease. We si una Malaria? Hata mimi si ni addict? Mimi pia
naumwa. Kwahiyo mimi mwenyewe nikienda Muhimbili pale nasema I am an
addict, I am sick, ukisema an addict ni kwamba you are sick.
Watu wengi wana mentality kwamba ‘huyu amejitakia mwenyewe’. Sio, ni
ugonjwa, akishaingia ameumia akitaka kutoka anashindwa. Kwahiyo ni
ugonjwa kama ugonjwa mwingine na unatibika kama ugonjwa mwingine.
Kwahiyo mimi nimeenda Muhimbili kama mgonjwa, nimewaambia tatizo langu
ni hili madaktari wa akili, madaktari wa sijui hivi wamenitibu mimi
nimepona kama mgonjwa mwingine, addiction is a disease.
Mimi na madawa sikujitakia, haujui nimeingiaje ndugu yangu usiniseme
mimi mwenyewe nataka kutoka nashindwa. Naamka asubuhi miguu inaniuma.
Naumwa kama mtu wa kansa. Viungo vyote vinaniuma, nafanyeje? Nipate
kidogo ili nipone lakini si kwamba napenda.”
Isikilize interview nzima hapa
Post a Comment