BW.SAED KUBENEA MKURUGENZI WA GAZETI LA MWANAHALISI
..........................................................................................................................................................................................................
Ongezeko
katika mashambulizi yaliyopo dhidi ya sehemu ya sheria kandamizi, na udhibiti
wa muda mrefu wa gazeti moja la kukosoa unachangia hofu na udhibiti binafsi miongoni
mwa waandishi wa habari nchini Tanzania, Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari
ilisema katika ripoti
mpya iliyotolewa leo.
Licha ya sifa nzuri ya Tanzania ya uwazi
na demokrosia, wananchi wayo wananyimwa taarifa muhimu.
"Mashambulizi ya hivi majuzi ya
waandishi wa habari, pamoja na sheria zinazopinga vyombo vya habari,
zinawafanyya maripota kuhofia zaidi usalama wao," alisema Tom Rhodes, mshauri
na mwandishi wa ripoti wa CPJ Afrika Mashariki. "Udhibiti wa binafsi una maana
ya kutoridhishwa kusikorekodiwa."
Ripoti, inayoitwa "Shida
Isiyoonekana ya Vyombo vya Habari vya Tanzania," inataja mwiba katika mashambulizi
na vitisho kama hivyo mwaka uliopita-CPJ imeweka kumbukumbu 10 za miezi
11 iliyopita-ikiwa ni pamoja na polisi kumwua mwanakamera mkongwe alipokuwa akiangazia msafara wa
upinzani.
Hakuna
afisa yeyote aliyewajibishwa kwa mauaji hayo ,Ripoti pia inaulizia taswira ya kimataifa ya serikali ya Tanzania kuhusu
kujitolea kwa uwazi na demokrasia, ikisema kuwa angalau sheria 17 zinazohusu
ukandamizaji wa vyombo vya habari zingalipo.
Chini ya sheria hizi, gazeti moja
la kukosoa, MwanaHalisi, limeondolewa kwa muda
usiojulikana, hatua ambayo waandishi wengi wa habari wanaiona kama ujumbe
unaotumwa kwenye mashirika yote ya vyombo vya habari.
Serikali imeahidi kurekebisha sheria za vyombo vya habari
na imetia sahihi kwenye Mradi Huru wa Ushirikiano wa Serikali, juhudi za pamoja
za kukuza uwazi.
Ilhali baada ya miaka mingi ya majadiliano, haijatoa sheria ya
kutekeleza ufikiaji wa taarifa au kubadilisha sheria mbalimbali zilizopo zenye
vikwazo.
Kama mojawapo ya mapendekezo muhimu ya ripoti, CJP
inasisitiza kuwa serikali inastahili kushauriana na vyombo vya habari na waandishi
wa habari ili kutunga na kutekeleza sheria ya kufikia taarifa inayohakikisha
kuwa wananchi wana ufikivu mpana wa nyaraka za umma.
Inastahili kuondoa
vipengele na sheria zote zinazonyima uhuru wa vyombo vya habari na kuondoa
marufuku na kuondoshwa kwa muda kwa vyombo vya habari. Uchunguzi wa kina wa
mashambulizi kwa waandishi wa habari lazima ufuatiliwe, ili wahusika washtakiwe
kwa mujibu wa sheria.
"Hatua za nidhamu za serikali ya Tanzania kuhusu uhuru wa
vyombo vya habari na kujieleza ni ishara tosha kuwa inahisi kutishwa
tunapokaribia uchaguzi wa urais na ubunge 2015," Rhodes alisema.
"Lakini ili
kutimiza viwango vya kimataifa vya uwazi na demokrasia, lazima serikali
iwaruhusu waandishi wa habari kuripoti kuhusu kile kinachoendelea nchini bila
hofu ya matokeo hasi."
IMETOLEWA NA
CPJ ni shirika huru, lisilo la faida linalofanya
kazi ili kulinda uhuru wa vyombo vy habari duniani kote.
Nairobi, Agosti 6, 2013-
|
Post a Comment