Serikali yapokea mizinga ya Kisasa 200 ya ufugaji nyuki

Serikali wilayani Sikonge mkoani Tabora imesema itaendelea kuhifadhi na kulinda mazingira ya asili katika pori la akiba la Ugala kwa ajili ya shughuli za utalii na ufugaji nyuki kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hiyo na Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu, kwenye makabidhiano ya mizinga mia mbili ya kisasa ya ufugaji nyuki yenye thamani ya shilingi milioni 24 iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Friedkin Conservation Fund (FCF) ambalo linajishughulisha katika uwindaji na utalii.

Mkuu huyu wa wilaya amesema wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyopakana  na mapoli ya akiba hawana budi kuendelea kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanahifadhiwa kikamilifu kwa manufaa yao.

Katika hutuba yake mkuu wa wilaya ya Sikonge ameritaka shirika hilo kusaidi vifaa vya kisasa vya ulinaji asali kwa wananchi hawa, Bw Nelson Kuwai ambae ni meneja mahusiano na maendeleo ya jamii wa shirika la Friedkin Conservation Fund amesema wanaowajibu wa kusaidi vifaa hivyo kama ambavyo wamekuwa wakichangia miradi mingine ya maendeleo.

Awali akisoma taarifa mwana kikundi Cha Vikoba tumo Edward Joseph amesema kikundi hicho cha kuweka na kukopa kinakabiliwa na changamoto mabali mbali za kiuchumi ikiwa pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiliamali.


Pamoja na shuhguli za uhifadhi shirika la Friedkin Conservation Fund na washirika wake wamekuwa wa kichaingia shughuli za maendeleo za vijiji ambavyo vinapakana na poli la akiba la ugala ili kuboresha maisha ya wananchi hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post