Sheikh achomwa kisu akiendesha ibada ya Idd - Mbeya

Mbeya — WAUMINI wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika ibada ya Swala ya Idd El Fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo Wilayani Kyela mkoani Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya Shekhe wao aliyekuwa akiongoza ibada kuvamiwa kibla wakati akiendesha ibada na kujeruhiwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea majira ya asubuhi ambapo Shekhe huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nuhu Mwafilango alishambuliwa akiwa katikati ya sijida baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela, Ally Mwangosi kuchoma Shekhe huyo na kitu chenye ncha kali.

Taarifa kutoka msikitini hapo zinadai kuwa mara baada ya tukio hilo, Shekhe alipiga kelele wa kuomba msaada na ndipo waumini waliokuwa wakiswali msikitini hapo waliposhikwa na taharuki.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Wilayani Kyela Bw. Daudi Mwenda alisema kuwa waumini walimuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Bw. Mwenda alisema kuwa Shekhe huyo ameumizwa vibaya kichwani na kutokwa na damu nyingi. Waumini wawili waliojaribu kumuokoa Shekhe huyo nao walijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu ikiwa ni pamoja na mweka hazina wa BAKWATA wilaya Ustadhi Khamis Hussein ambaye alijeruhiwa kichwani na sikioni.

Nao baadhi ya waumini waliokuwepo katika ibada hiyo walisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati waumini wote wakiwa wamesujudu, ndipo waliposikia kelele na vurugu.

Mmoja wa waumini aliyejitambulisha kwa jina la Idd Hussein alisema kuwa liliibuka kundi la watu waliomsaidia kijana huyo, na kuibua vurugu kubwa iliyosababisha ibada ya swala ya Idd kuvunjika.

Akizungumzia tukio hilo Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Shekhe Juma Killah alisema kuwa vurugu hizo zimetokea katika swala ya Idd na wahusika wa vurugu hizo ni  Waislamu ambao...   Read more

Post a Comment

Previous Post Next Post