JARIBU
KUJIULIZA ni jina la single mpya ya Kala Jeremiah kutoka jiji la Miamba
Mwanza inayotegemewa kutoa Jumatano wiki ijayo (August 14).
Katika wimbo huo ambao umepikwa na mtayarishaji Nahreel wa Hometown
Records, Kala ameunganisha ukomavu wake wa tungo na sauti ya msanii wa
kike Mary Lucoss ambaye pia ni zao la shamba la Madam Ritha (BSS).
Kwanini Mary Lucos na siyo msanii mwingine wa kike? Hata Kala
mwenyewe ‘alijaribu kujiuliza’ ni msichana gani anayeweza kufit vizuri
katika wimbo huu, wazo la mwanzo Kala alihitaji kupata sauti ambayo
haijazoeleka sana na baada ya mchakato bahati ilimdondokea Mary
atakayesikika katika kiitikio cha wimbo huo.
Wimbo huu utaanza kutoka audio na baadaye video itafuata

Post a Comment