Kama
wewe si mtazamaji wa filamu za kibongo huenda sura ama jina la Skyner
Ally ni geni kabisa. Au labda mara yako ya kwanza kumuona msichana huyu
mrembo ni kwenye video ya Bob Junior ya wimbo wake Kimbiji.
Skyner Ally Seif ni kipaji kilichogunduliwa na Ray na tayari
ameshaigiza kwenye filamu kadhaa zikiwemo ‘The Second Wife’, ‘What is
It’, ‘Why I Did Love’, ‘I Hate My Birthday’, ‘Kizungumkuti’,
‘Unpredictable’ na sasa yupo location akiigiza kama mke wa Ray kwenye
filamu mpya, Chicken Head.

Skyner kwenye set ya Chicken Head
Skyner ambaye aliolewa mwaka 2011 na aliyezaliwa mwaka 1992, ametokea
kupata umaarufu kwenye fani hiyo na kwa muonekano wake Jacky Wolper na
Irene Uwoya wakae chonjo.
Post a Comment