
Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hoteli ya New Africa jijini
Dar kuhusiana na msimu mpya wa ligi za soka katika SuperSport. Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu Meneja Mauzo Salum Salum pamoja na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi.

Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kulia)
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema
DStv imezidi kusogeza huduma kwa wateja wake ambapo hivi karibuni
imefungua tawi jipya Kariakoo barabara ya Msimbazi na kuongeza kuwa
kuanzia sasa Channel ya SuperSport itakuwa ikionekana katika eneo lote
la kusini mwa jangwa la Sahara.

Meneja
Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) akizungumza na
wanahabari ambapo amewataka wananchi kujiunga na huduma za DStv kwani
bei zake ni nafuu na picha zake zinaonekana katika kiwango bora.
Kama
mtu ni mteja aliyeunganishwa na DStv, sasa atapata msisimko zaidi
akisikia kuwa kuanzia mwezi huu wa Agosti SuperSport’s football
itawaletea mambo mengi na mazuri zaidi.
Katika
msimu mpya, SuperSport itawaletea michapo yote inayohusu soka la
Uingereza kwa sasa ambapo kocha mtata Jose Maurinho amerejea katika Ligi
Kuu ya Uingereza.
Kama
vile hiyo haitoshi pia Bundesliga itakuwa ikionekana katika SuperSport
pekee katika eneo lote la Kusini mwa Jangwa la Sahara itakuwa ni ligi
nyingine itakasisimu katika msimu mpya.
Kwa
sasa Ligi hiyo ndio inayopewa kiwango cha juu barani Ulaya kufuatia
mafanikio ya timu za Bayern Munich na Borussia Dortmund katika msimu
uliopita wa michuano ya Ligi ya UEFA na sasa wanatamba kuwa na moja ya
meneja mwenye mafanikio katika kipindi cha miaka mitano Pep Guardiola.
SuperSport ni mahali pekee kutazama ligi mbalimbali za soka.
Ligi
hizo ni pamoja na English Premier League (EPL), Spanish La Liga,
Italian Serie A, German Bundesliga, UEFA Champions League, UEFA Europa
League, South African Premier Soccer League (PSL), Kenya Premier League
(KPL), Uganda Super League (USL), Nigerian Premier League (NPL), Angolan
Girabola, Ghana Premier League, Zambia Premier League na CAF Champions
League.
Post a Comment