Swala
la kulala vitanda tofauti kwa wapenzi linaweza kuwa na tafsiri mbaya
kwa wapendanao lakini utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa matokeo
yake yana faida zaidi ya hasara katika mahusiano.
Utafiti uliofanywa Ryerson University huko Toronto, Canada, umeonesha
kuwa kati ya asilimia 30 na 40 ya wanandoa hulala vitanda tofauti
usiku, na wataalamu wanasema kujitenga wakati wa kulala kunaweza kuwa na
faida zaidi katika kusaidia kuimarisha uhusiano zaidi ya madhara yake.
Colleen Carney, mwandishi wa utafiti huo aliiambia CBS kuwa, wanandoa
(couples) wanaolala pamoja huwa hawapati kiwango cha usingizi
kinachotakiwa. Badala yake hua wanajikuta wanaamshana mara kwa mara kwa
milio mbalimbali (mikoromo) na kujigeuza mara kwa mara.

Aliendelea kusema kuwa wapenzi wanapaswa wafikirie juu ya kulala
tofauti kwa faida ya kupata mapumziko bora ya usiku na kuboresha
mahusiano.
Carney pia alizungumzia dhana iliyozoeleka kuwa wanandoa au wapenzi
wakilala tofauti basi wanakuwa wamegombana kwa kusema kuwa ‘Watu
wanaweza kuwa na uhusiano mzuri sana na wa kuridhisha kwa kulala mbali
mbali, watu wengine wanaweza hata kuwa wanaelekea kupeana talaka lakini
kwa kulala tofauti inaweza kusaidia wakarudisha mapenzi yao’.
Alitoa mfano wa wapenzi wa Canada walioishi kwa kulala vitanda tofauti kwa miaka 14 na mpaka sasa ni wanandoa wenye furaha.

Post a Comment