Serikali ya Zimbabwe imekanusha madai kuwa imeiuzia Iran madini ya urani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, afisa wa serikali ya Zimbabwe
amekanusha ripoti ya gazeti la 'Times' la Uingereza ambalo lilidai kuwa
Zimbabwe imetia saini mkataba wa kuiuzia Iran madini ya urani.
Naibu Waziri wa Madini Zimbabwe Gift Chimanikire amenukuliwa akisema
nchi yake haijatia saini mkataba wowote wa kuiuzia Iran madini ya
urani.
Katika mahojiano na tovuti ya Bloomberg, Chimanikire alisema Zimbabwe
haina uwezo wa kutosha wa kuhamishia urani katika nchi zingine.
Ameongeza kuwa makubaliano yaliyotiwa saini na Iran yanahusu sekta
mbalimbali za madini kama vile almasi n.k. Madini ya urani aghalabu
hutumika katika vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia
Post a Comment