Ziwa Rukwa kufungwa miezi 6; Ziwa Nyasa kuchunguzwa kuhusu hofu ya kombora

Ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya linatarajiwa kila mwaka kufungwa kwa miezi sita kwa lengo la kutoa fursa kwa samaki kuzaliana na kukua.

Katibu tawala wa wilaya hiyo akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kasi ya kutoweka kwa samaki katika ziwa hilo  ambapo hivi sasa wavuvi wanavua samaki wachanga ambao hawafai kwa kitoweo. 

Matukio ya samaki kufa katika ziwa Nyasa yamezua hofu kwa wananchi kwamba huenda nchi ya Malawi imetupa kombora ziwani huku Malawi nao wakiwa na hofu kama hiyo kwamba huenda Tanzania imetupa
fataki kutokana na ugomvi wa nchi hizo kugombea ziwa Nyasa, na hivyo serikali imesema itatuma watalaamu kuchunguza sababu za samaki hao kufa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dk Therezya Huvisa akizungumza na wananchi kadoni mwa ziwa Nyasa wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Ruvuma alisema, “Nimepata taarifa kuwa samaki wanaokufa katika Ziwa Nyasa sasa wameleta hofu kwa wananchi wa nchi zote mbili Tanzania na Malawi, kwa hiyo ninachoweza kuwaambia ni kwamba tutatuma wataalamu kuchunguza chanzo cha samaki kufa. Lakini pia kuna wavuvi wanatumia majani yanayoitwa mtunungu kuvulia samaki ambayo ukimwaga ziwani au mtoni samaki wanakufa, kwa hiyo msitumie sumu kuvulia samaki. Hao wanakufa ziwani humo bila kujua chanzo chake msiwale.”


TOA MA

Post a Comment

Previous Post Next Post