AFYA:- HATARI YA KUWEKWA MAFUTA MENGI KTK VYAKULA~

~~~HATARI YA KUWEKWA MAFUTA MENGI KTK VYAKULA~~~
 ( Kula kiafya – kula vizuri na njia inayofaa)
 A/Alleykum;
 Kula vizuri kunahusu kufanya uamuzi unaofaa kila mara. Lengo lako liwe tu kula lishe bora lenye virutubishi vyote visivyo na mafuta mengi na ambavyo si vya kunonesha. Pia ni muhimu uchunge kiasi cha chakula unachokila. Usiweke tu mlima wa chakula kwenye sahani yako!.
 NI vizuri kuwa mwangalifu na kila kitu tukitumiacho katika maisha yetu ya kila siku. Pamoja na kuwa mambo yote hupangwa na Mwenyezi Mungu, uvunjaji wa taratibu alizotuwekea ndio hupelekea kwenye hukumu zote.
 
Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini. Mwili huwa hatupi kinachofaa, badala yake kama hakitumiki wakati huo, huhifadhiwa kwa baadaye. Ndio maana tunapokula vyakula vyingi vyenye mafuta mengi hutupelekea kuongeza unene na uzito.
 Tatizo la unene huwa ni chanzo cha magonjwa mengi mengine. Kwani eneo kubwa ya damu (High Blood pressure) hutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo hupelekea mirija ya kusafirisha damu kuwa na mafuta. Hii husababisha njia ya kupitia damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini kama inavyotakiwa. Nguvu hii ya ziada huongeza au kupunguza mapigo ya moyo. Yanapoongezeka sanani hatari na yanapungua sana ni hatari pia. Hivyo tusinenepe sana. Vilevile matatizo haya huambatana na matatizo mengine ya moyo.
 
Mafuta mengi huleta madhara hasa kwa wagonjwa wa kisukari. Mafuta na sukari huwa ni chanzo kizuri cha nguvu mwilini. Vinapokuwa pamoja, kila mmoja wao anataka awe yeye wa kwanza kutoa nguvu mwilini, kwa wagonjwa wa kisukari, sukari zao zinakuwa ndogo hushindwa kugombania nafasi na mafuta iwapo yatakuwa mengi. Hivyo ni vyema kuwapunguzia wagonjwa wa kisurikari mafuta mengi kwenye vyakula.
 
Mafuta mengi kwenye vyakula pia huzuia ufyonzwaji wa madini ya calcium mwilini. Kazi za madini ya calcium ni nyingi sana, mfano kukunja na kunyooka kwa viungo, mifumo ya ufahamu, uimara wa mifupa na meno, n.k. Hivyo basi tusile kupita kiasi bali kidogo tu. 

Mafuta yanapozidi kwenye vyakula husababisha tumbo kujaa, kwani uyayushaji wa vyakula vyenye mafuta mengi huchukua muda mrefu ukilinganisha na vilivyo na mafuta machache. Vilevile huzuia kutolewa kwa vimeng'enyo(enzymes) muhimu za uyeyushaji na hivyo kuchelewesha kazi ya usagaji. Mara nyingine husababisha kuharisha ambako hupoteza maji na virutubisho vingine. 

Mafuta mengi hukinaisha mlaji. Hii husababisha mtu kuacha kula mapema hata kabla hajashiba au kula vile anavyohitajiwa kula. Ni muhimu kupunguza mafuta kwenye vyakula vya watu wasio na hamu nzuri ya kula. Mfano wagonjwa, watoto, wazee sana, wajawazito, au wafanyakazi waliochoka sana. Wengi wao huwaletea kichefuchefu na hata kutapika au kuua kabisa hamu yao ya kula.
 
Mafuta mengi mwilini huweza kusababisha magonjwa ya kibofu (gallstones) kutengeneza vijiwe kwenye kibofu ambavyo ni hatari kwa afya. 

Ni vyema kuyatumia mafuta kama kiungo muhimu katika vyakula lakini si kama chakula kikuu. Na ni bora kutumia mafuta yatokanayo na mimea (kama alizeti, pamba, chikichi n.k.) kuliko yatokanayo na wanyama. Mafuta yatokanayo na wanyama yana (cholesterole) ambayo ni hatari kwa magonjwa mengi, mfano ya moyo na kibofu. Mwili una uwezo wa kutengeneza cholesterole yake kwa kiwango kinachohitajika. Tunapozidisha ndio tunaishia kwenye maadhara badala ya faida.
 ......Shukraan Wabillahy towfiq
HATARI YA KUWEKWA MAFUTA MENGI KTK VYAKULA~~~

Post a Comment

Previous Post Next Post