Kamanda Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga. |
AIRTEL kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini mwaka huu yadhamini
tena uchapishaji wa Stika za usalama barabarani katika kuadhimisha wiki
ya usalama barabarani nchini, Moblog inaweza kuripoti.
Airtel imetajwa kuwa moja kati ya makampuni ambayo yamekuwa
yakishirikiana na serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na
tatizo la ajali za barabarani.
Akithibitisha maelezo hayo, Kamanda Mkuu wa kikosi cha usalama
barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel imeweza kutoa
mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa
ikitoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na kikosi cha
usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha ajali za barabarani.
“Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani, kwa miaka
mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa
wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia imedhamini vipindi vya
elimu ya usalama barabarani katika TV – kumekucha na Jambo Tanzania
(ITV na TBC 1) na Radio one.
Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na jeshi la polisi usalama
barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu=
Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati
wakiendesha magari.
Vile vile mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa
wapanda pikipiki (Bodaboda) yaliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya
usalama barabarani kwa waendesha pikipiki ,” amesema DCP Mpinga.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania Bi Beatrice Singano
Mallya, akizungumza juu ya suala hilo, amesema “Airtel imeamua
kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la
ajali za barabarani. Idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa mno
na ndiyo maana Airtel imeamua kujikita katika kuokoa maisha ya wateja
wake na watanzania kwa ujumla. Tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa
swala la kupunguza ajali za barabarani ni wajibu wa kila mwananchi
hivyo tutii sheria bila shuruti”
Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani
katika kuhakikisha lengo letu la kupunguza ajali linafanikiwa, tumeanza
kuona mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabaranizinapungua
kulinganisha na miaka iliyopita,” alisema Beatrice.
Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu wiki ya nenda kwa usalama
barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza kupungua kwa kiasi
kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana nao katika
programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea mwaka 1995
ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000 na 4,000.
Lakini Mwaka 2010 ukilinganisha na 2011 ajali zilipungua kwa 3% na 2011
na 2012 ajali zilipungua kwa 2%.
Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini wiki hii ambapo kwa mwaka huu
imejitolea kuchapisha tena stika za usalama barabarani pamoja na
kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha bodaboda
yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono juhudi
za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa elimu
kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote ili
kuepusha ajali.
Chanzo - MOBLOG
Post a Comment