
Cheka amelimbia gazeti la Mwananchi kuwa hakupata nafasi ya kuendelea
na shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba,
ila kwasasa ameamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule
ya St Joseph.
“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo
hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee
na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine“. Alisema cheka.
Mpiganaji huyo wa masumbwi pia amefunga kiwanda cha kusaga chupa
nyumbani kwao Morogoro baada ya kununua mashine ya milioni 8 hali
iliyosaidia kuajiri vijana wasio na kazi zaidi ya ishirini na tano.
Post a Comment