Wananchi wa Rwanda kipiga kura |
Na Ali Bilali
Chama cha RPF cha Rais wa Rwanda Paul Kagame kinaelekea kupata ushindi
wa kishindo katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika jana nchinihumo na
ambao unaendelea leo kwa kuwachaguwa wawakilishi 24 wa kike. Uchaguzi
huo umeanza jana jumatatu na unaelekea kutamatishwa kesho baada ya
kuchaguliwa wa wawakilishi watatu wa walemavu.
Muungano wa vyama unaoongozwa na Chama cha RPF cha rais Paul Kagame
unaelekea kupata ushindi katika uchaguzi huo ambapo kiasi ya kura ambazo
zimekwisha hesabiwa chama hicho kimejipatia asilimia 76 ya kura baada
ya matukio ya awali ya uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa matokeo yaliwekwa bayana na tume ya kitaifa ya uchaguzi
NEC, Chama cha RPF na washirika wake wamepata kura 3.395.962 kati ya
4.462.917 zilizo pigwa. Wananchi wasiofikia milioni sita walikuwa
wamejiorodhesha katika daftari la wapiga kura ambapo mkuu wa NEC Kalisa
Mbanda anasema kuwa matukio hayo ya awali ni sawa na asilimia 60 ya
wapiga kura.
Chama cha PSD kimepata asilimia 13.01 huku chama cha PL kikipata asilimia 9.38 ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa.
Chama cha PS-Imberakuri kinachukuwa nafasi ya tatukwa asilimia 0.56 ya
kura kikkifuatiwa na wagombea binafsi wanne wote wakiwa na asilimia 0.5
ya kura.
Vyama vya RPF, PSD na PL ndivyo ambavyo vitakuwa na wawakilishi bungeni
ambapo ndivyo vinazidi asilimia 5 ya kura inayoagizwa ili viwakilishwe
bungeni
kutokana na tofauti iliopo na idadi ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa, matokeo hayo huenda yasibadiliki sana.
kwa mujibu wa tume ya kitaifa ya uchaguzi NEC, huenda pasiwi na
mabadiliko makubwa ya matokeo hayo, kura za raia wa Rwanda wanaoeshi nje
ya nchi ndizo pekee ambazo zinaweza kubadili matokeo.
Wachambuzi wa maswala ya siasa wanasema kuwa Vyama vya PSD na PL ambavyo
vinashiriki katika serikali ya rais Kagame ni vibaraka wa chama tawala
ambavyo vipi kwa ajili ya kubaini kuwa kuna mfumo wa vyama vingi nchini
Rwanda.
Chama cha PS-Imperakuri cha rais wa zamani Bernard Ntaganda alieko
korokoroni tangu mwaka 2010 kwa tuhumu za kutaka kuyumbishas usalama wa
taifa na ubaguzi, nacho pia kinashukiwa kimepata ulaghai kutoka chama
tawala cha RPF.
Matokeo ya sasa hayapishana sana na yale ya mwaka 2008 ambapo chama cha
RPF kilipata asilimia 78.7 ya kura dhidi ya asilimia 13.12 ya chama cha
PSD na asilimia 7.5 ya chama cha PL.
Chanzo - kiswahili.rfi.fr
Post a Comment