Na Said Ameir, Ikulu
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ametoa wito kuendelezwa tafiti zaidi juu ya historia ya uislamu Zanzibar
ili kuweka kumbukumbu sahihi za kipindi ulipoingia na namna ulivyoingia
nchini.
Dk.
Shein ametoa wito huo leo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la
Kimataifa Kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu Katika Afrika ya
Mashariki linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya La Gema huko
Nungwi, Mkoa wa Kakazini Unguja.
Aliwaeleza
washiriki wa kongamano hilo kuwa kumbukumbu za historia ya uislamu
Zanzibar zinaonyesha simulizi tofauti kuhusu mwaka ulioingia na namna
ulivyoingia hivyo ipo haja historia hiyo muhimu kufanyiwa tafiti zaidi
ili kupata kumbukumbu sahihi.
“Kwa
msingi huo, nashauri utafiti zaidi uendelee kufanywa kuhusiana na
historia ya Uislamu hapa Zanzibar na fani mbalimbali zinazohusiana na
utamaduni wa kiislamu ili tuweze kubaini mwaka halisi ambapo Uislamu
uliingia Zanzibar na namna ulivyoingia” Dk. Shein alisisitiza.
Kuhusu
mchango wa Zanzibar katika kukuza na kueneza ustaarabu wa kiislamu
katika maeneo ya Afrika Mashariki Dk. Shein alieleza “masheikh na
maulamaa mbalimbali wa Zanzibar walikwenda kueneza uislamu katika maeneo
mengine kama vile Tanzania bara, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na
wengine walifika Komoro na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Kaskazini na baadhi ya nchi za Asia”.
Aliongeza
kuwa wananchi wa Zanzibar wanapata faraja kuona taarifa za Zanzibar
zinatumika na kuthaminiwa katika kuelezea mchango wake kwa ajili ya
kuendeleza ustaarabu wa kiislamu na mafundisho ya dini hiyo katika
ukanda wa Afrika ya Mashariki.
Ili
kuendeleza na kuhifadhi historia ya Uislamu katika ukanda huo Rais wa
Zanzibar alitoa rai kwa waandaaji wa kongamano hilo na wadau wengine
kuangalia uwezekano wa kuanzisha kituo cha historia na utamaduni wa
kiislamu wa kanda hiyo Zanzibar na kueleza kuwa Serikali iko tayari
kutoa ushirikiano unaostahiki kufanikisha rai hiyo.
“Serikali
yangu iko tayari kutoa ushirikiano wa kila hali iwapo hili (la
kuanzisha kituo cha historia na utamaduni wa kiislamu) litazingatiwa na
kuona umuhimu wake kwa lengo la kulitekeleza”alisema.
Katika
hotuba yake hiyo Rais wa Zanzibar alitambua mchango mkubwa wa lugha ya
Kiswahili katika kueneza ustaraabu na mafundisho mengine ya dini ya
kiislamu.
“Lugha
ya Kiswahili imekuwa ikitumika ikiwa kama chombo muhimu cha kueneza
ustaraabu na mafundisho mengine ya dini ya kiislamu kupitia mawaidha,
darsa na pia tafsiri za vitabu vya dini”alieleza na kutolea mfano
tafsiri ya Quran tukufu ya Sheikh Abdalla Saleh Al- Farsi aliyewahi kuwa
Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Dk. Shein aliwaeleza
washiriki wa kongamano hilo kuwa matarajio ni kuona kongamano hilo
linatoa mchango mkubwa na muhimu kitaaluma na kuongeza maarifa kuhusu
historia ya ustaraabu wa kiislamu kwa washiriki na watu wengine ambao
watapata fursa ya kufuatilia kongamano hilo.
“kwa
hivyo tuhakikishe kuwa elimu hii inawafikia kwa kutambua kuwa elimu ni
amana na neema waliyopewa waja kutoka mwa Mola wao na hivyo ni wajibu
wao kuwafikishia wengine kama walivyofanya maulamaa na masheikh wetu
mbalimbali ambao baadhi yao tumewataja”alisisitiza.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini mchango wa unaotolewa na
taasisi za kidini na ndio maana imeanzisha Ofisi ya Mufti kusimamia
masuala ya kidini.
Dk.
Shein alihimiza pia mshikamano na umoja miongoni mwa waislamu na katika
kusimamia na kuendeleza dini yao kwa kuwa hawapaswi kabisa kuhasimiana
hasa kwa misingi ya dini na imani.
Aliwakata
wananchi wa Zanzibar kulinda ustaarabu wa kuendesha mihadhara ya
kumarisha dini, kusimamia amani na umoja na mapenzi miongoni mwa
waislamu kama walivyofanya viongiozi wa dini waliotangulia.
Wakati huo huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amefisu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ufalme wa Oman.
“napenda nitambue uhusiano mzuri na udugu uliopo kati ya Serikali na wananchi wa Zanzibar na Serikali
ya Ufalme wa Oman na watu kwake ” Dk. Shein waliwaeleza washiriki wa
Kongamano la Kimataifa Kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu Katika
Afrika ya Mashariki na kumtakia kila la heri kiongozi wa Ufalme wa Oman
Sultan Qaboos.
Post a Comment